NDIZI aina ya koroboi
imekuwa ni ndizi Muhimu kwa Wananchi wa Micheweni, pichani gari ya abiria ya
Micheweni ikipakia ndizi hizo kutoka katika gari ya Mkoani
NDIZI mbivu aina ya
Mkono mmoja ni bidhaa muhimu kwa futari katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani, kidole kimoja kinauzwa kati ya 1000, 1500, 2000 hadi 2500, mkungu
mmoja unauzwa kati ya 20000/= hadi 25000/=.
BIDHAA za Nafaka
zimeonekana kuwa nyingi katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, huku
baadhi yake bei zikionekana kuwa chini, ila njugu mawe imeweza kupanda hadi
kufikia 3500/- kutoka 25000/=
MMOJA wa wachukuzi wa
mizigo katika soko la Matunda na Mboga mboga Chake Chake, akiwa amebeba mikungu
ya ndizi katika kiroba kwa lengo la kupeleka mnadani katika soko hilo
MMOJA ya
wafanyabiashara wa nazi katika soko la Tibirinzi Chake Chake, akiwa napanga bidhaa
zake ambapo fungu moja la nazi nne linauzwa 3000/=
NDIZI aina ya Mkono mmoja na mtukwe ikionekana kwa wingi katika
soko la matunda na mboga mboga Chake Chake, baada ya kuteremshwa kutoka katika
gari na kusubiri kupigwa mnada.(Picha na Abdi Suleiman -Pemba)
No comments:
Post a Comment