Habari za Punde

Tetesi za Soka Ulaya : Mikel Arteta atakuwa meneja wa Arsenal?

Mikel Arteta alijiunga na Arsene Wenger Arsenal kutoka Everton mwaka 2011 na akastaafu 2016.16
Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na Mikel Arteta amekubali kuteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ya England. (Goal.com)
Iwapo Arteta, ambaye kwa sasa ni mkufunzi msaidizi Manchester City ataondoka Etihad na kwenda Emirates, Pep Guardiola anapanga kumchukua kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona na Uhispania Andres Iniesta, 34, kama mchezaji mkufunzi. (Yahoo)
Kipa wa Manchester City Joe Hart, ambaye aliachwa nje ya kikosi cha England kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia atakuwa anatafutwa na Southampton na Wolves baada ya West Ham kuamua hawamtaki kwa mkataba wa kudumu. Hart, 31, amekuwa West Ham kwa mkopo. (Mirror)
Leicester wanataka kumchukua beki wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 30, kutoka West Brom, lakini huenda ada ya £4m inayodaiwa na wakala wake ikawa kikwazo. (Mail)
Stoke City wanataka aliyekuwa meneja wa West Ham David Moyes awe meneja wao mpya baada ya Paul Lambert kuondoka klabu hiyo iliposhushwa daraja hadi ligi ya Championship. (Sun)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.