Habari za Punde

Kombe la dunia 2018: Jezi ya Nigeria yauzwa yote baada ya watu milioni 3 kuagiza

Nigeria huenda sio wanaopigiwa upatu kushinda kombe la dunia lakini wanaonekana kupata mashabiki wengi kupitia jezi yao mpya.
Mashabiki milioni 3 tayari wameagiza tisheti kama hizo kulingana na shikisho la soka la Nigeria na wanunuzi walipanga foleni nje ya duka la kampuni ya jezi ya Nike mjini London siku ya Ijumaa ili kujaribu kununua nguo hizo.
Tisheti hizo zilizokuwa zinauzwa kwa bei ya £64.95, ziliuzwa katika tovuti ya kampuni ya Nike muda mfupi baada ya kutolewa.
Kiungo wa kati wa Arsenal Alex Iwobi ni miongoni mwa waliouza jezi hizo ambazo zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Februari , pamoja na mchezaji wa Leicester Wilfried Ndidi, ambaye alivaa kofia na jaketi katika picha za kampeni ya kuziuza jezi hizo.
Nigeria inatarajiwa kuvaa jezi hizo mpya wakati itakapokabiliana na Uingereza katika mechi ya kirafiki ya kombe la dunia katika uwanja wa Wembley Jumamosi Usiku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.