Habari za Punde

Wimbo mpya wa Diamond unaomshirikisha Zari 'Iyena' wazua hisia

Wimbo mpya wa nyota wa muziki wa bongo Diamond Platinumz kwa jina 'Iyena' unaomshirikisha mfanyibiashara wa Uganda na mama wa watoto wake wawili Zari Hassan umezua hisia kali.
Wimbo huo ambao ni wa pili katika albamu yake ya ABoyFromTandale kwa jina IYENA unaomuhusisha msanii Rayvanny unamuonyesha mwanamuziki huyo akifunga ndoa na Zari Hassan licha ya wawili hao kuwachana.
Kanda hiyo ya video ilio na mandhari ya ndoa ilirekodiwa wakati wawili hao walipokuwa pamoja.
Katika wimbo huo Platinumz anaonekana akifunga ndoa na mama wa watoto wake wawili huku Rayvany na Fahyma wakiwa wasimamizi wakuu wa harusi hiyo.
Baadhi ya mashabiki walidhania kwamba wimbo huo ulikuwa wa ishara ya msani huyo kurudiana na Zari Hassan
Katika wimbo huo Platinumz anamuhakikishia Zari kwamba 'talaka ndio njia ya mwisho atakayokuwa akifikiria baada ya kufunga ndoa'.
Image captionMfanyibiashara na raia wa Uganda Zari Hassan
Hivi ndivyo msanii huyo alivyoandika katika mtandao wake wa twitter kabla ya kutoa kibao hicho:
Na punde tu baadaye mashabiki wake walituma ujumbe katika mtadao wa twitter wakijibu.
Hatahivyo kuna wale waliokerwa na msanii huyo kutoa wimbo huo mwezi mtukufu wa Ramadhan
Zari na Diamond waliwachana mwezi Februari mwaka huu baada ya kuwa pamoja kwa takriban miaka mitatu.
Zari alisitisha uhusiano wao siku ya wapendwanao ya Valentine kwa kuchapisha ua jeusi na ujumbe mrefu kwa Diamond akisema amechoshwa na 'tabia' ya mwanamuziki huyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.