Habari za Punde

Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani Laadhimisha Zanzibar Katika Ukumbi wa Watu Wenye Ulemavu Welesi



 Mwanaharakati Zanzibar Bi.Asha Aboud akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani,yakiadhimishwa leo Zanzibar Katika Ukumbi wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Welesi Zanzibar,imewashirikisha Wadau na Azaki Kiraia Zanzibar. Yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar,Juwauza,Zgc,Actionaid Kwa Ufadhili wa DANIDA.
 Mwanaharakati Bi. Salma Sadat akitowa Mada kuhusiana na Mtoto Mwenye Ulemavu kukosa haki zake za msingi.
Mwanaharakati Mhe. Jamila Mahmoud akiwasilisha Mada yake ya Uchunguzi wa Watoto Wenye ulemavu katika hatua zao za kupata mahitaji yao ya msingi katika kupata elimu ya msingi na sekondari iliofanywa na Azaki za Kiraia.
Wanaharakati wakifuatilia Mada zinazowakilisha wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Umoja wa Walemavu Welesi Kikwajuni Zanzibar.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.