Habari za Punde

Maandalizi wa Ujenzi wa Mabanda ya Sikukuu Katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo.

Ujenzi wa Mabanda ya Biashara katika Uwanja wa Mpira Mnazi Mmoja ukiendelea kujiandaa na maandalizi ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry inayotarajiwa kufanyika kesho iwapa utaandama mwezi kukamilisha mfungu wa mwezi wa Ramadhan, unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii. Duniani kute na kuungana Waislam kusherehekea Eid El Fitry. 

Wafanyabiashara katika viwanja vya mnazi mmoja wakisubiri kugawiwa sehemu zao za Biashara ya Taasisi husika ya Manispa ya Zanzibar kwa ajili ya kufanya biashara katika viwanja hivyo wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry  baada ya kuandama kwa mwezi leo au kesho.
Wafanyabiashara ya michezo ya Watoto katika viwanja vya Sikukuu vya Mnazi mmoja wakijenga na kufunga pembea katika viwanja hivyo kwa ajili ya Watoto watakaofika katika viwanja hivyo kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry mwishoni mwa wiki hii.
Wafanyabiashara ya michezo ya Watoto katika viwanja vya Sikukuu vya Mnazi mmoja wakijenga na kufunga pembea katika viwanja hivyo kwa ajili ya Watoto watakaofika katika viwanja hivyo kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry mwishoni mwa wiki hii.
Askari wa Usalama Barabarani wakiwa  katika mazoezi ya kuongoga msafara  wakati wa kuingia katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, kama wanavyoonekana wakiingia katika eneo hilo wakati wa mazoezi hayo leo.
Watoto wakiwa katika moja ya Salon za kunyolea nywele kwa ajili ya kujiandaa la sikukuu ya Eid El Fitry mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.