Habari za Punde

Harakati katika Mitaa ya Mji wa Zanzibar Kujianda na Sikukuu ya Eid El Fitry Inayotarajiwa Kusherehekewa Kwa Kuandma Kwa Mwezi Mwishoni Mwa Wiki Hii Baada ya Mfungu wa Mwezi wa Ramadhan.

Wananchi Kisiwani Zanzibar wakiwa katika harakati za kujipatia mahitaji yao katika Marikiti Kuu ya Darajani Unguja kwa ajili ya kukamilisha matayarisho ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry inayotarajiwa kufanyika kesho au keshekutwa ikiwa mwezi utaandama leo, 
Mandari ya barabara ya darajani ikiwa na msongamano wa magari na wananchi wanaofika katika marikiti kuu ya darajani kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa mbalimbali. 
Muonekano wa Mtaa wa Darajani mchana huu wananchi wakiwa katika harakati kwa ajili ya maandalizi ya Sikukuu ya Eid El Fitry.Inayotarajiwa kufanyika kesho iwapo mwezi utaandama leo jioni na kuungana na Waislamu wengine Duniani kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitry.  
Eneo maalum la maegesho ya magari lililotengwa kwa ajili hiyi kwa Wananchi wanaofika katika Marikiti Kuu ya Darajani kufuata mahitaji yao mbalimbali, maegesho hayo hutumika kwa kiwango cha malipo ya shilingi 1000/= kwa siku.
Wananchi Kisiwani Zanzibar wakiwa katika harakati za kutimiza vifaa vya maandalizi ya matumizi ya Sikukuu ya Eid El Fitry inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii baada ya mfungu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Wananchi Kisiwani Zanzibar wakiwa katika harakati za kutimiza vifaa vya maandalizi ya matumizi ya Sikukuu ya Eid El Fitry inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii baada ya mfungu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Wafanyabiashara ya Nyama katika Marikiti Kuu ya Darajani wakiwa katika harakati ya kutowa huduma hiyo kwa wateja wao wanaofika katika marikiti darajani kupata nyama kwa ajili ya matumizi kilo moja ya nyama leo imeuzwa shilingi 12,000/= kwa kilo moja tafauti na siku mbili za nyuma ilikuwa ikuuzwa shilingi 8500/= na 9000/=

Wafanyabiasha ya Kuku Visiwani Zanzibar wakiwa katika eneo la marikiti Kuu ya Darajani wakisubiri wateja wao Kuku mmoja ameuzwa shilingi 12,000/= Kipindi hichi kuku wamepanda bei kutoka shilingi 6500/= hadi bei hiyo inayosababishwa na mahitaji zaidi kwa ajili ya Sikukuu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.