Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohamed Shein Amefanya Uteuzi wa Taasisi Mbalimbali..

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa
Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Bibi Hamida Ahmed Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara ya Zanzibar katika Wizara ya Biashara na Viwanda.

2. Bwana Omar Ramadhan Mapuri ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia, Zanzibar.

3. Bibi Mwanamkaa Abdulrahaman Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.

4. Dr. Abdul-Nasser Hamed Hikmany ameteuliwa kuwa Mrajis wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira.

5. Bwana Salum Kitwana Sururu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho na Mambo ya Kale katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 14 Juni, 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.