Waziri
wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa
Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/19 Bungeni Jijini Dodoma ambapo
kwa mwaka 2017 uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia 7.1.
Baadhi
ya viongozi na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia
kwa makini Taarifa ya Hali ya Uchumi
wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/19 iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), Jijini
Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb), wakifurahia jambo Bungeni Dodoma baada ya
kuwasilishwa kwa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka
2018/19 ambapo vipaumbele vya sasa ni
pamoja na mazingira wezeshi ya ufanyaji wa biashara, viwanda vya kukuza uchumi
na kufungamanisha ukuaji wa uchumi na Maendeleo ya watu.
Kamishna wa Bajeti wa Wizara ya
Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya
Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) Bw. Pius Maneno
(wa pili kulia) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bw. Mohamed Mtonga, wakiwa katika viwanja vya
Bunge Jijini Dodoma baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango, kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka
2018/19.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango, Bi. Susana Mkapa, (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara
ya Fedha na Mipango Bw. William Mhoja wakipeana
mikono katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma baada ya
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb), kuwasilisha
Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa
Taifa wa mwaka 2018/19 ambapo Tanzania
kwa mwaka 2017 mfumuko wa bei ulikua kwa wastani wa asilimia 5.1.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens
Luoga, akizungumza jambo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke
baada ya Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa
katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/19. ambapo moja
ya vipaumbele vya sasa ni Kuimarisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakibadilishana mawazo katika viwanja vya
Bunge Jijini Dodoma baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango, kuwasilisha Taarifa ya
Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/19 ambapo Serikali imetenga
takribani Sh. trilioni 12 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo.
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments:
Post a Comment