Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ajumuika katika Iftar na Wananchi wa Chakechake Pemba Ikulu Ndogo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemedi Suleiman (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Mhe.Rashid hadid Rashid mara baada ya Swala ya Magharibi jana kabla ya Futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini  Pemba jana katika Futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar kabi
Baadhi ya  Mashekhe wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pembaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar
Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake,Wilaya ya Chakechake ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akijumuika na Viongozi akinamama na Wananchi wengine wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar
Baadhi ya Akinamama wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chake chake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein amefutari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Futari hiyo imeandaliwa na Alhaj Dk. Shein kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba ilifanyika katika Ikulu ndogo Chake Chake, ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini, vyama vya siasa, Serikali pamoja na wananchi wa Mkoa huo.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein nae alishiriki kikamilifu katika hafla hiyo ya futari akiwa pamoja na viongozi wanawake wa Kitaifa na wananchi wengine wa Mkoa huo.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Rais Dk. Shein, Mkuu wa Mkoa huo Hemed   Suleiman Abdalla aliwataka wananchi kuendeleza amani, utulivu, umoja na mshikamano pamoja na kuendelea kuiombea dua nchi yao  ili iendelee kupata neema.

Alieleza kuwa mafanikio makubwa yataendelea kupatikana hapa nchini iwapo mashirikiano ya pamoja yatakuwepo  na wananchi wote wataendelea kuwa kitu kimoja.

Alieleza kuwa nafsi zote zikiwa pamoja basi Mwenyezi Mungu ataendelelea kuleta neema na kuwasisitiza wananchi Waislamu na wasiokuwa waisilamu kuendelea kuiombea dua nchi, viongozi pamoja na kuwaombea wananchi wote.

Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kutoa mashirikiano wakati wote kwa shughuli zote za Serikali na za kijamii kwenye maeneo yao kwa ajili ya kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwao.

Sambamba na hayo, aliwataka wananchi kuendelea kupiga vita vitendo vyote viovu kwa maslahi yao pamoja ili jina la Zanzibar liendelee kutajika vyema.

Alitoa shukurani kwa wananchi wote waliofika katika kufutari pamoja kwa kuungana na Rais Dk. Shein kwa ajili ya kufanya kitendo hicho cha ibada hasa katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein aliwashukuru wananchi pamoja na viongozi wote wa dini na vyama vya siasa waliohudhuria katika futari hiyo aliyowaandalia na kupongeza jinsi walivyoonesha upendo mkubwa kwake wa kukubali muwaliko wake huo.

Mkuu huyo wa Mkoa pia, alimpongeza Alhaj Dk. Shein kwa kitendo chake hicho cha kufutarisha na kueleza fadhila na ujira mkubwa anaopata mtu anaefutarisha wenziwe na thamamani ya kufutarisha.

Pia, walimuombea dua Alhaj Dk. Shein kuendelea kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu na kumuomba Mwenyezi Mungu ili kiongozi huyo aendelee kuwafanyia mazuri kama aliyowafanyia ambapo yote hayo yatakuwaja iwapo wote watakuwa wamoja.

Nao wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba wakitoa neno la shukurani lililotolewa na Sheikh Mohammed Suleiman kwa niaba yao walitoa shukurani kwa futari nzuri aliyowaandalia na kuonesha furaha yao kwa kufutari pamoja kiongozi wao huyo.

Kwa niaba ya wananchi hao, Sheikh Mohammed alieleza kuwa watu wema wanajuana kwa alama njema na Alhaj Dk. Shein ana alama njema kwani kuna dalili zote kuwa yeye ni Mcha Mungu, mnyeyekevu na amekuwa akimuogopa Mwenyezi Mungu pekee yake.

Sheikh Mohammed alieleza kuwa ni neema ya kuwa na kiongozi kama huyo huku akitumia fursa hiyo kumuombea dua ili Alhaj Dk. Shein aendelee kuwa na afya njema.

Aidha, alieleza kuwa Alhaj Dk. Shein amekuwa karibu sana na raia wake na amekuwa haangalii wapi anapotoka ama kabila alilonalo na badala yake amekuwa akiwasaidia  wananchi wake wote bila ya kinyongo wala ubaguzi.

Sheikh Suleiman alimsifu Rais Dk. Shein kwa niaba ya wananchi wa Mkoa huo kwa kufanya kitendo hicho cha kuwafutarisha katika kumi hili la mwisho la Ramadhani ambalo linaubora na umuhimu mkubwa katika suala zima la ucha Mungu.

Leo Rais Dk. Shein anatarajiwa kufutari pamoja na wananchi wa Jimbo la Mkanyageni huko katika viwanja vya skuli ya Mkanyageni.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.