Habari za Punde

Sheha aliedaiwa kumpiga mkewe, atakiwa kutoa fedha za matibabu haraka….

Na Haji Nassor, PEMBA
MAMA mzazi, wa mke wa sheha wa shehia ya Chimba wilaya ya Micheweni Hamad Ayoub Khamis, amemtaka mkwe wake, kutoa  haraka gharama za matibabu ya mke wake, ili kumtibu maumivu ya mwili anayoendelea kuyaaguza, baada ya kutolewa hospitali ya Wete hapo juzi.
Mama huyo, alisema kwa vile bado mkewe huyo, hajamuacha mwanawe, hana budi kuendelea kutoa huduma kamili, ikiwemo suala la matibabu hasa kwa vile yeye peke yake, hamudu gharama hizo pamoja na kumpatia chakula.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mama huyo, alisema hakuna jinsi kwa mkwe, juu ya kumsaidia gharama za matatiba, maana mwanawe alimuia sana kutokana na majeraha alioyapata, akiwa mikononi mwake.
Alieleza kuwa, kwa sasa hahitaji vikao vya kujadili sababu ya mwanawe kupigwa, au chanzao cha ugomvi wao, bali cha msingi ni kwa mkwewe, amabe ni sheha wa shehia ya Chimba kuchangia gharama za matibabu, ili kijana wake apone.
Alisema yeye atapokea fedha za matibabu kutoka kwa muume wa mwanawe, maana haoni sababu ya kukataa kwa vile yeye peke yake, uwezo wa kumtibu hanao hasa kwa vile anao watoto watano anaowahudumia.
“Ni kweli mimi sijapokea takala kutoka kwa mkwe wangu, kwamba mwanangu amemuacha, sasa kwanza sina muda wa kushughulikia ugomvi wao, nnachohitaji achangie gharama, maana ndani ya siku nne nashamutumia shilingi 100,000,”alifafanua.
Alisema licha kwamba wameshatolewa hospitali ya Wete walikokuwa wamelazwa, lakini bado mwanawe hajaweza kutembea na hulazimika kusota anapokwenda chooni, na goti la mkuu wa kulia liko hali mbaya zaidi.
Alifafanua kuwa, kama alimkabidhi mwanawe akiwa mzima na sasa wameshazaa nae watoto watano, lazima afikirie ubinaadamu na kuona kumsaidia gharama za matibabu haraka sana.
“Dawa nyengine hulazimika kununua, hivyo fedha za kila siku mimi na familia yangu ni shida, na pia Juni 14, natakiwa kumrejesha tena hospitali, sasa fedha mimi ntazitolea wapi,”alieleza.
Katika hatua nyengine mama huyo mzazi, amesema uamuzi wa kumrejesha au kutomrejesha mwanawe kwa mume wake huyo, atakuwa nayo muolewa husika, hasa baada ya kupona majeraha aliyoyapata.
“Mimi mwanangu akisema anataka kurudi tena kwa mume wake, sina tatizo, maana siwezi kumzuia mke wa mtu, lakini lazima na sisi familia tukutane, maana tulimpa mke waendeshe maisha na sio kufanya ngoma,”alifafanua.
Kwa upande wake muume wa wanamke Hamad Ayoub Khamis, ambae ni sheha wa shehia ya Chimba, alisema yeye suala la kumtibu mke wake wala hasubiri kuhimizwa na mkwewe, na anayo nia hiyo.
Alisema Juni 11 anatarajia kwenda ukweni kwake Kipangani Wete, na akitarajia kulala huko huko, ambapo pamoja na mambo mengine, lengo ni kutoa fedha za matibabu, kwa ajili ya mke wake.
“Mimi mama mkwe hana haja ya kuniomba suala la matibabu ya mke wangu, na hata huduma nyengine, ni wajibu wangu, maana bado huyu ni mwanamke sijamuacha na wala sina lengo hilo, tumeshazaa watoto watano sasa,”alieleza sheha huyo.
Katika hatua nyengine, ameendelea kushikilia msimamo wake na kumuomba Muumba, iwapo mwanamke huyo alinyanyua kitu chochote na kumpiga, kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.
“Mimi sijampiga, na bado nashangaa kusikia hivyo, kama kweli nimempiga kwa tendo alilolifanya, na pia kungetanguliwa na takala, lakini bado namtaka mke wangu,”alieleza.
Alidai kuwa, kilichojitokeza, wakati anampapatua na mwanamme waliokuwa wakivuuka maadili, ndipo alipoanguka na kushutka mguu, lakini sio kwamba alimpiga rungu kama ilivyoelezw.
Hata hivyo mwanamke huyo, hapo juzi akizungumza na waandishi wa habari, alikiri kupigwa na mume wake, akidai bila ya kisa, ambacho anakikumbuka kikifanya, bali ni kwa chuki zake za muda mrefu.
Tayari jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, limeshamuhoji na kumuachia kwa muda, sheha huyo baada ya jeshi hilo kupokea tuhuma za mwanamke mmoja kupigwa na mume wake huyo Juni 4 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.