Habari za Punde

Ujerumani Watupwa Nje ya Kombe la Dunia 2018.

Baada ya kuwaliza mbele ya mashabiki wa nyumbani wakiwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2002, Ujerumani nayo imepata kuhisi uchungu wa kutolewa Kombe la Dunia.
Mabao ya Son Heung-min dakika ya 96 na Kim Young-gwon dakika ya 91 yametosha kuidhalilisha Ujerumani na kuitema kutoka Dimba la Dunia.
Aidha, Ujerumani yenye mazoea ya kuwadunisha wengine, imeadhibiwa pia kufuatia unyama iliyowatendea Brazil 2014 kwa kuwafunga 7-1 mbele ya mashabiki wa nyumbani.
Ujerumani imejiunga na Ufaransa, Italia na Uhispania kuwa mabingwa waliochujwa kutoka taji walicholenga kulitetea.
Die Mannschaft waliingia mchuano huo ukiwa wa mwisho, wakipigiwa upatu kwa kuwa na nafasi nzuri ya kufuzu kutoka hatua ya makundi.
Walipojumuishwa Kundi F, wengi walihisi ni mteremko kwa timu hiyo yenye mastaa, Mesut Ozil na Toni Kroos.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.