Habari za Punde

Wanamuziki Kutoka TAMUFO Watinga Viwanja Vya Bunge Dodoma na Kuzungumza na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais wa Umoja  wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga nje ya viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo wakati wa ziara ya wanamuziki hao kutembelea Bunge kuona shughuli zinazofanyika.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwanamuziki Mkongwe Mzee Makasy, wakati wa ziara hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza mwenyeji wa wanamuziki hao Mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata (kulia). wakati akitoa maelezo kuhusu ziara ya  wanamuziki  hao Bungeni.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, akisalimia na mwanamuziki, Mzee Makassy. Kulia ni Mwanamuziki  Kikumbi Mwanza Mpango (King Kiki)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwanahabari Dotto Mwaibale ambaye ameongoza na wanamuziki hao katika ziara ya kutembelea Bunge.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Katibu wa TAMUFO. Kulia mwenye koti jeupe ni Mwanamuziki, Hamza Kalala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimia na mwanamuziki, Kikumbi Mwanza Mpango (King Kiki)  na wasanii wenzake  katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma  leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba.Kutoka kushoto ni Rais wa TAMUFO, Dk. Donald Kisanga, mwenye kofia nyekundu ni Mzee Makassy na Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata .  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wanamuziki hao.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki hao.

Na Mwandishi Wetu

WANAMUZIKI waliopo kwenye  Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), leo wameshuhudia shughuli mbalimbali zinazofanyika Bungeni katika ziara yao ya kutembelea Bunge.

Katika ziara hiyo  wanamuziki kutoka makundi mbalimbali kama ya muziki wa Injili, Dansi, Asili, Bongo Fleva na Taarabu yalikuwepo na hiyo ndiyo dhima ya umoja huo wa kitaifa.

Wakiwa katika viwanja vya Bunge wanamuziki hao walibahatika kukutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi wengine akiwepo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifurahi kuwaona wanamuzi hao na akawakaribisha siku nyingine.

Rais wa TAMUFO, Dk.Donald Kisanga  alisema ziara hiyo kwao ni ya kihistoria kwani imekuwa ni ya mapokezi makubwa kuanzia kwa Waziri Mkuu, Wabunge, Mawaziri na Mwenyeji wao Mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata.

"Kwetu ziara hii imetupa taswira mpya tumeweza kuona jinsi wabunge wanavyouliza maswali ya kuwakilisha wananchi hakika kama TAMUFO ni jambo la kujivunia" alisema Kisanga.

Katika hatua nyingine Kisanga ametoa shukrani zake kwa uongozi mzima wa Kanisa Kuu la Anglikana na jijini Dodoma kwa mapokezi waliyotoa kwao tangu wafike mkoani humo mwishoni mwa wiki hadi siku ya kuondoka kwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.