Habari za Punde

CCM yatoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya Mil 17 shule ya msingi ya Wazazi

 VITABU vilivyotolewa na uongozi wa CCM Mkoa wa mjin
  WANAFUNZI wa Shule ya msingi ya Wazazi wakisoma utenzi uliokuwa na ujumbe unaohusu mafanikio, changamoto na hatua za kimaendeleo za shule hiyo
 BAADHI ya waalikwa mbali mbali wakiwemo wazee, walezi, walimu na  viongozi wa Chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioudhuria katika hafla hiyo ya makabidhiano.
 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib, akihutubia katika hafla hiyo na kuelezea kwa upana utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib(kulia),akimkabidhi vitabu vya kusomea na kufundishia Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi  Khamis Kheir Ame (kushoto), hafla hiyo ilifanyika Amani katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mjini kimekabidhi vitabu 2,415 vyenye thamani ya shilingi milioni 17 kwa  inayomilikiwa na taasisi hiyo.
Vitabu hivyo ni miongoni mwa mwendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020,inayotekelezwa kwa kasi na kwa ufanisi mkubwa katika jamii.
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini uliopo Amani Zanzibar.
Talib alisema utoaji wa vitabu hivyo ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Chama katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita kwa kuimarisha sekta mbali mbali za umma, hasa elimu ambayo ndio nyenzo muhimu ya kuharakisha maendeleo ya nchi.
Aliwataka walimu wa shule hiyo kuvitunza na kusimamia vizuri matumizi ya vitabu hivyo ili wanafunzi waweze kupata muda mrefu wa kusoma na kupata uelewa mpana wa masomo yao.
Pia alieleza kuwa shule hiyo imekuwa na historia ya kushika nafasi bora za ufaulu katika mitihani ya taifa, hivyo walimu, wazee na walezi wanatakiwa kuendeleza ushirikiano wa malezi ya pamoja kwa lengo la kuendeleza sifa hiyo ya ufaulu kwa wanafunzi hao.
“Vitabu hivi ni vya masomo yote yanayofundishwa katika shule hii natarajia vitapunguza ama kumaliza kabisa changamoto ya ukosefu wa vitabu, na wanafunzi watapata kusoma kwa bidii.
Dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ni kuimarisha miundombinu ya shule ya Wazazi iwe ya kisasa na yenye kutoa elimu bora kwa watoto ambao ndio viongozi na wataalamu wa fani mbali mbali wa baadae.”, alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha aliahidi kuhakikisha shule hiyo inapata usajili wa ngazi ya sekondari ili wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi waweze kujiunga moja kwa moja na shule ya sekondari.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Khamis Kheir Ame alitoa shukrani kwa uongozi wa CCM Mkoa wa mjini kwa busara na ubunifu wao wa kutoa msaada wa vitabu kwa taasisi hiyo ya kitaaluma.
Alisema msaada huo unathamani kubwa sana katika sekta ya elimu kutokana na umuhimu wake unaomwezesha mwanafunzi kupata nyenzo ya kujifunzia wakati wowote akiwa shuleni ama nyumbani.
Akisoma risala mwalimu wa shule hiyo, Swaum Othman Juma alizitaja changamoto zinazowakabili katika shule hiyo kuwa ni pamoja na upungufu wa madawati, kuchelewa kwa usajili wa shule ya sekondari pamoja na walimu hao kupewa mshahara  ndogo usiokidhi mahitaji yao ya kila siku

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.