Habari za Punde

Mwanamke 'aliyekufa' apatikana hai Afrika kusini katika jokofu

Mwanamke mmoja Afrika kusini anapokea matibabu hospitalini baada ya kupatikana akiwa hai katika jokofu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Mwanamke huyo alifikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha serikali baada ya madaktari kusema amekufa kufuatia ajali ya barabarani, na kutoonyesha dalili zozote za uhai, gazeti la TimesLive linaripoti nchini.
Familia ya mwanamke huyo aliyegunduliwa kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti inasema wamepata mshtuko na wana wasiwasi mkubwa kuhusu mkasa huo.
Jamaa mmoja kutoka familia hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina ameiambia BBC kuwa wamepata mshtuko mkubwa lakini wanahitaji ufafanuzi wa ni vipi makosa kama hayo yanaweza kutokea.
Huku hayo yakiarifiwa, mwanamke huyo ambaye hakutajwa ili kumlinda, anapokea matibabu katika hospitali ya Leratong magharibi mwa mji wa Johannesburg.
ramani
Alisemekana kuwa amekufa kufuatia ajali ya barabarani Jumapili lakini wakati mfanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti alipofika kuutizama mwili na kutayarisha nyaraka kumhusu - aligundua kwamba bado mwanamke huyo anapumua.
Mamlaka ya afya katika eneo hilo imeazisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.
Mkurugenzi wa kampuni ya kuitikia matukio ya dharura - Distress Alert operations - ilioshughulikia kisa hicho inasema 'hakuna ushahidi wa utepetevu' kwa niaba ya kampuni yake.
"Hili halikutokea kwasababu wahudumu wetu hawakupewa mafunzo vizuri," aliliambia gazeti la TimesLive.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.