Habari za Punde

Nafasi za Kazi Shirika la Umeme ZECOShirika la Umeme Zanzibar (ZECO) linakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika kada mbali mbali kwa waombaji wenye sifa stahili kwa ajili ya Unguja na Tawi la Pemba kama ifuatavyo:

 UNGUJA 

1 MHANDISI UMEME (ELECRTICAL ENGINER)    Nafasi- 2.
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata  shahada au stashahada ya juu  ktk fani ya umeme (Degree or advance diploma in Electrical Engineering or Electrical and Electronics Engineering).
© Umri usiozidi miaka 40 ifikapo mwezi wa august,2018
© Awe na Ujuzi wa kutumia kompyuta

2 FUNDI MCHUNDO ( ELECTRICAL TECHNICIAN) -Nafasi 2
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata  stashahada ktk fani ya umeme (Ordinary diploma in Electrical Engineering).
© Umri usiozidi miaka 30 ifikapo mwezi wa august,2018
© Awe na Ujuzi wa kutumia kompyuta.

3 FUNDI SANIFU (ARTISIAN) -
Nafasi 1
Sifa za muombaji
©Awe amehitimu na kupata cheti cha elimy ya sekondari ( form 2 or form4 ) 
© Awe amehitimu na kupata cheti cha VETA.
© Umri usiozidi miaka 30 ifikapo mwezi wa Agost,2018.

4 DEREVA ( DRIVER ) -Nafasi 2
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya sekondari ( form 2 or form 4)
© Awe na leseni hai ya udereva
© Umri usiozidi miaka 30 ifikapo mwezi wa agost 2018
© Ujuzi wa ufundi ni sifa ya ziada.

5 MTUNZA GHALA (STORE KEEPER )

- Nafasi 1

Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata Stashahada katika fani ya manunuzi na ugavi( ordinary diploma in procurement and logistic management/material management).
© Umri usiozidi miaka 40 ifikapo mwezi wa Agost 2018
© Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

 PEMBA 

1 FUNDI SANIFU (ARTISIAN) -
Nafasi 1
Sifa za muombaji
©Awe amehitimu na kupata cheti cha elimy ya sekondari ( form 2 or form 4 ) 
© Awe amehitimu na kupata cheti cha VETA.
© Umri usiozidi miaka 30 ifikapo mwezi wa Agost,2018.

 JINSI YA KUTUMA MAOMBI. 

Muombaji anatakiwa kuandika barua ya maombi na akiambatanisha na vitu vifuatavyo

@ Barua ya sheha wa shehia anayoishi muombaji
@ Vivuli (photocopy) vya vyeti vya kumalizia masomo , kitambulisho cha mzanzibari na leseni kwa atakaeomba nafasi ya udereva.
@ maelezo binafsi (curriculum vitae ) ya muombaji.
@ Kila muombaji anatakiwa kuainisha juu ya bahasha nafasi anayoiomba .

Maombi yanaweza kutumwa kwa lugha ya kiswahili au kiingereza.

Mazingatio;

Muombaji anasisitizwa kuandika namba yake ya simu  na namba ya mtu wake wa karbu ktk barua yake ya maombi kwa mawasiliano.

Maombi yote lazima yatumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo.

MENEJA MKUU,
Shirika la Umeme,
S.L.P 235,
Zanzibar.

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 13/julai 2018

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.