Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mandisi Robert Gabriel, akiendelea na ziara yake kutembelea miradi ya maendeleo kujionea utekelezaji wake katika kufanikisha umaliziaji wake.
Mhe. Mandisi Robert
Gabriel ameendelea kufuatilia hatua za utekelezaji wa Miradi mbalimbali Mkoani
Geita kwa kufanya ziara na kuona miradi inayotekelezwa kwa fedha za Huduma kwa
Jamii (CSR) kutoka Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM).
Ametembelea
na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mzunguko wa Kisasa (Round About) inayojengwa
Halmashauri ya Mji wa Geita. Awapongeza mafundi, ashauri ujenzi uendelee siku
zote ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.
Mhe.
Mandisi Gabriel amesema na wasimamizi wa mradi kwa kusema, ‘zingatieni thamani ya fedha (Value for
Money) na ubora, lakini pia ikibidi mnara unaojengwa ukamilike kabla ya mwaka
kuisha kwa kuwa sisi waandisi tukiwa na sikikuu nchi haitajengwa’. Pia
amesifu usanifu wa mchoro wa Mnara utakao kaa katikati ya Round About hiyo ukiwa
na uwakilishi wa vitu mbalimbali mfano alama ya Mwenge wa Uhuru (uwakilishi wa
taifa letu), Matofali ya Dhahabu (alama ya utajiri wa madini) lakini pia
itakuwepo saa ambayo inaonyesha kiwango cha joto.
Kwa
upande mwingine, Mhe. Mandisi Gabriel ameushukuru
uongozji wa Mgodi wa GGM baada ya kutembelea na kuona jumla ya mifuko ya saruji
2,136 iliyopelekwa Halmashauri ya
Mji Geita katika utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu na Afya kisha kujionea hatua ya
uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kisasa inayoanza kujengwa
eneo la Magogo lililotengwa kwa ajili ya Shule. Mkuu wa Mkoa kwa mara nyingine
akasema; angependa kuona ujenzi wa Shule hiyo inaanza mara moja, maboma
yakamilike ndani ya miezi mwili na nusu, kisha ukamilishaji ufuatie na yeye
atashiriki kwa kuwa msimamizi wa shughuli ya ujenzi akizingatia thamani ya
fedha hivyo aliwataka wananchi kuanza usafi mara moja kwani tayari baadhi ya
vifaa vya ujenzi kwa nguvu za wananchi vipo kwenye eneo hilo.
Mkuu
wa Mkoa alisisitiza kwa kusema, “kwa kuwa
tunatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama
Tawala CCM, na kwa kasi ninayoiona, tukikaa vizuri kufikia mwakani, Zahanati
kila Kijiji tunamaliza kabla ya Uchaguzi Mdogo wa mwaka 2019 kwani maboma
yakikamilika tutakuwa juu ya asilimia 80 upande wa Sekta ya Afya. Hata kwa upande wa elimu, maendeleo siyo
mabaya” aliongeza.
Alipofika
Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mhe.Mandisi
Gabriel aliona mifuko 680 ya
saruji na kupokea taarifa iliyoeleza kuwa bado mifuko 1,459 haijawasilishwa na kwamba kufikia wiki ijayo itakuwa imefika.
Lakini pia aliagiza ujenzi uanze wiki
inayofuata kwakuwa anapanga kutembelea utekelezaje wake.
Miongoni
mwa alioambatana nao katika ziara hiyo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita,
Mhe. Herman C. Kapufi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita pamoja na
wawakilishi wa Mgodi wa Dhahabu Geita GGM
No comments:
Post a Comment