Habari za Punde

Wanavikundi Vya Ushirika Zanzibar Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Umakini na Uwazi Kujinusuru na Migogoro.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,Wazee, Wanawake na Watoto bi Maua Makame Rajabu amewataka Wana vikundi vya ushirika Zanzibar kufanya kazi kwa umakini na uwazi ili kujinusuru na migogoro inayoweza kujitokeza.
Amesema bado kuna baadhi ya Wananchi wamekuwa na dhana potofu ya kuingia katika vyama vya ushirika ni kuibiana jambo ambapo halina ukweli hivyo iwapo watakuwa wawazi na wakweli dhana hiyo itaweza kuondoka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika afisi ya Idara ya vyama vya ushirika Migombani Wilaya ya Mjini  kuhusiana na maandalizi ya siku ya ushirika inayofanyika kila mwaka Jumamosi ya mwanzo wa mwezi wa saba amesema ushirika umeweza kuwakomboa watu wengi kutokana na tatizo la umasikini kwa kuchukuwa mikopo na kufanyabiashara,kilimo ,mifugo na ujasiriamali.
Amesema ni kweli kuna baadhi ya Viongozi wamekuwa wakianzisha vyama vya ushirika na kuviweka mikobani jambo ambapo linapelekea baadhi ya wanachama kutokuwa na imani na viongozi hao na kupelekea migogoro katika vyama hivyo.
Ameweka wazi kuwa Serikali imechoka kusikia migogoro ya vyama vya ushirika na kupelekea kuibiana jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa hali na mali.
Amesema suala la ushirika linaingia katika maeneo mawili makuu ikiwemo eneo la uzalishaji katika nyanja kama vile kilimo, mifugo na biashara.
Amesema lengo la kuanzishwa kwa Idara ya maendeleo ya vyama vya ushirika Zanzibar ni kuweza kuwanyanyua Wananchi kwa kujipatia kipato kwa kusomesha watoto wao, kujenga nyumba na kukopa na kuendesha maisha yao.
Kwa upande wake Afisa kutoka Idara ya maendeleo ya vyama vya ushirika Zanzibar Zuhura Suleiman Ali amesema tokea kuanzishwa kwa vyama vya ushirika wananchi wengi wameweza kujipatia kipato na kuweza kuendesha maisha yao kupitia nyanja mbali mbali za kiuchumi.
            Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.