Habari za Punde

Watumiaji Mitandao ya Kijamii Uganda Hawana Pa Kujifichia Kukwepa Kodi ya Serikali.

Watumiaji mitandao ya kijamii Uganda hawana mahala pa kujificha kukwepa tozo la kodi ya mitandao ya kijamii iliyoidhinishwa na serikali.
Agizo jipya limetolewa kwa makampuni ya mawasiliano Uganda kuzuia mfumo unaoruhusu watumiaji mitandao kuweza kuingia katika mitandao hiyo -VPN - ambao baadhi ya wateja sasa wanaitumia kuvuka vizuizi vilivyowekwa kuwaruhusu kuingia katika mitandao hiyo ya kijamii na kukwepa kulipa Kodi.
Sasa serikali imesema hilo linaelekea kwisha. Wanachi watakuwa hawana njia ya kukwepa kulipa kodi ya mtandao.Serikali inasema hatua hiyo itasaidia kuingiza kipato kinachohitajika pakubwa, lkini wanaharakati wanaikosoa hatua hiyo kuwa ya jaribio la 'kubana' uhuru wa kuzungumza.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la wiki, Weekly Observer, mkurugenzi mtendaji wa tume ya mawasialiano Uganda, Godfrey Mutabazi, kampuni za simu zitaanza kuzuia taratibu programu tumishi za mfumo wa VPN unaowasaidia Waganda kukwepa kulipa kodi ya mitandao ya kijamii.


Rais Yoweri Museveni alishinikiza mageuzi hayo , akieleza kuwa mitandao ya kijamii huchangia kuenea kwa udaku nchini.
Agizo hilo la kulipa kodi kwa mitandao kama Whatsapp, Facebook, Twitter na kadhalika, limeanza kufanya kazi tarahe mosi Julai nchini.
Kumeibuka hisia mchanganyiko miongoni mwa raia Uganda wengi wakieleza walivyoathirika nalo, huku wengine kwa shingo upande wakilipa kodi hiyo.
Hii ni mifano ya waliofanikiwa kuingia katika mitandao ya kijamii ambao walitumia fursa kuelezea hisia zao kuhusu agizo hilo jipya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.