Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Adhimisha Siku ya Mashujaa Kwa Kushiriki Katika Usafi wa Mazingira Eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam ambako Julai 25, 2018 waliadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy baada ya kuwasili katika eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam  kuadhimisha siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo hilo 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  wakifyeka nyasi kwenye  eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam  wakati waliposhiriki  katika maadhimisho ya   Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipeleka uchafu kwenye gari la takataka wakati waliposhiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la Coco Beach  baada ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye  eneo hilo Julai 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la Coco Beach baada ya kushirika katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo Julai 25, 2018. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia mti alioupanda baada ya Kuadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salam Julai 25, 2018. Kushoto ni mkewe Mary na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakizungumza na Bibi Amina Fadhili (kulia) baada ya kuadhimisha siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira kwenye  eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya kukamua juisi ya miwa, mali ya Abdillah Issa (kulia) wakati alipotembelea eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam baada ya kuadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo hilo Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.