Habari za Punde

ZFDA Yaangamiza Tani 95 za Chakula na Tani Moja ya Dawa za Binaadamu Zilizomaliza Muda wa Matumizi.

 
SEHEMU ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.


SEHEMU ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.

FUNDI wa mageti akikata geti la Ghala lililokua likihifadhiwa bidhaa za Mchele, Unga wa ngano na sembe uliomaliza muda na haufai kwa matimizi ya Binadamu katika mtaa wa Migombani Mjini Zanzibar.
 SEHEMU ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
 GARI ya Kijiko likiuharibu kwa kuufukia Unga wa Ngano uliokua haufai kwa matumizi ya Binadamu katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 DAWA za binadamu za aina mbali mbali za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizo angamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
 GARI la Kijiko likiangamiza Dawa za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizoangamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
 MKURUGENZI Idara ya Udhibiti na Usalama wa Vyakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungamza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamizaji Bidhaa zisizofa kwa Matumizi ya Binadamu lililofanyika katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Abdalla Omar Maelezo  -  Zanzibar.

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar                16.7.2018
Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imejidhatiti 
kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinawafikia 
wananchi zikiwa salama kwa matumizi kwa lengo la kulinda 
afya zao.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula wa 
ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar alieleza hayo katika jaa la 
Kibele wakati wa kazi ya kuangamiza tani 95 za bidhaa za 
mchele, sembe na Unga wa ngano pamoja na tani moja ya 
dawa za binadamu.
Alisema bidhaa za chakula zilizoangamizwa za 
mfanyabiashara Mohamed Mattar ziliharibika baada ya 
kuhifadhiwa kwa muda mrefu katika maghala yasiyorasmi 
na yaliyokosa sifa za kutumika kwa kazi hiyo.
Dkt. Khamis alieleza kuwa kutokana na maghala hayo 
kukosa viwango vinavyokubalika na kutosajiliwa na ZFDA, 
mfanyabiashara Mattar alikuwa  akiweka bidhaa zake kwa 
siri wakati wa usiku.

Akitaja viwango vya bidhaa zilizoangamizwa, Mkurugenzi wa 
Idara ya Udhibiti na uhifadhi wa chakula wa ZFDA alisema 
mchele ulikua tani 52, unga wa ngano tani 37 na sembe 
ilikuwa tani sita.
Alisema sehemu ya bidhaa hizo zilikuwa zikitolewa kama 
sadaka katika mwezi wa Ramadhani kama mbinu ya 
mfanyabiashara huyo kujaribu kukwepa gharama za 
kuangamiziwa bidhaa zake.
Mkurugenzi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Chakula 
aliwataka wafanyabiashara wanapotaka kutoa sada ya 
chakula kuishirikisha ZFDA ili kuhakikisha ubora na usalama
wa bidhaa itakayotolewa.
Mfamasia wa ZFDA Nassir Buheti alisema kiwango kikubwa 
cha dawa zilizomaliza muda wa matumizi zilitoka Taasisi za 
kiraia (NGO) kwa ajili ya kuangamizwa  na kiwango kidogo 
kilipatikana katika maduka ya kuuzia dawa.
Buheti alitoa wito kwa maafisa wa NGO wanaopata msaada 
wa dawa kutoka nje kuwa waangalifu katika kuzitumia na 
inapokaribia miezi mitatu kabla ya kumaliza muda wa 
matumizi na wakihisi haziwezi kumalizika wazipeleka ZFDA 
ili wazisambaza katika vituo vya afya vya Serikali ambako 
mahitaji ya dawa ni makubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.