Habari za Punde

Fei Toto aanza kwa pasi 50 Yanga

IKIWA ni mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kiungo mpya wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, juzi Alhamisi alipiga pasi 50 katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kiungo huyo amejiunga na Yanga msimu huu kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea JKU ya Zanzibar.
Fei Toto
Katika mchezo huo ambao Fei Toto alianza kucheza namba kumi kabla ya Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kuumia ambapo alipo­toka Fei Toto akashuka chini na kucheza nafasi ya kiungo mkabaji ambapo alifanikiwa ku­piga pasi 25 tena akicheza kwa utulivu mkubwa.

Katika pasi hizo, 23 ndiyo zilifika kwa walengwa wakati pasi mbili zilipotelea njiani huku akipokonya mipira mara mbili tu kutokana na muda mwingi kutumia kukaba. Hiyo ni katika kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili, kiungo huyo alipiga tena pasi 25, akipoteza pasi tatu pekee na 22 zikifika kwa walengwa. Mbali ya pasi hizo alipokonya mipira mara tatu, akipiga shuti moja huku akicheza faulo mbili sawa na alizokuwa amechezewa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.