Habari za Punde

Jumia Yasisitiza Kuuza Bidhaa Bora na Halisi Katika Mtandao.

KATIKA kuwajengea Watanzania mazingira salama na rahisi ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao, Jumia imesisitiza kuwa bidhaa zote zinazopatikana kwenye mtandao wake ni halisi na zenye bora wa hali ya juu kutoka kwa kampuni na wafanyabiashara wanaoaminika Tanzania na duniani kote.

Kwa watanzania wengi dhana ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao bado ni ngeni na haijazoeleka. Miongoni mwa sababu zinazopelekea hali hiyo ni; uaminifu kwa sababu hakuna mawasiliano ya moja kwa moja baina ya muuzaji na mnunuzi, hofu ya wizi wa mitandaoni kutokana na upya wa huduma hii pamoja na changamoto ya maendeleo ya kiteknolojia ambayo watu wengi bado hawajafikiwa nayo.

Watanzania wengi wamezoea kwenda maduka moja kwa moja pale wanapohitaji kununua bidhaa kwa sababu hupata wasaa wa kuziona, kuzishika, kuzijaribisha, kufanya makubaliano ya bei ili kujiridhisha zaidi kabla ya kukata shauri la kununua.

Akizungumzia juu ya faida ambazo zimeletwa na mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao kwa wafanyabiashara na wateja wa Kitanzania, Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania, kampuni inayoongoza kwa huduma za manunuzi mtandaoni Afrika, Bw. Albany James amebainisha kuwa mfumo huu upo kwa ajili ya kuwarahisishia wateja huduma za kufanya manunuzi pamoja na kuongeza thamani kwa wafanyabiashara.

“Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanahofia pengine mfumo huu umekuja kuua biashara zao, la hasha! Maendeleo yoyote ya teknolojia duniani huja kwa lengo la kurahisisha maisha ya kila siku ya binadamu. Mfumo wa manunuzi ya mtandaoni una faida kubwa ya kuwa ni rahisi, kuokoa muda na gharama kwa mteja kwenda na kurudi dukani. Badala yake, mteja mahali popote na muda wowote alipo anaweza kuperuzi bidhaa, kununua na kisha kuletewa mpaka alipo,” alielezea Bw. James.

Kwa nchi kama Tananzania na nyinginezo zinazoendelea Afrika ambapo ufahamu na mwamko wa matumizi ya huduma za kiteknolojia bado ni mdogo, kunakuwa na ugumu katika kuyapokea mabadiliko kama ya manunuzi ya mtandaoni kwa haraka.

Ukiachana na maendeleo ya teknolojia, Watanzania wengi bado hawana ufahamu wa kutosha juu ya mifumo salama ya kufanya manunuzi mtandaoni hivyo kupelekea kuwa wagumu kuwaamini wafanyabiashara wanayojihusisha nayo.

“Jumia ni  tofauti na mitandao mingine inayodai inafanya huduma za manunuzi ya mtandaoni. Utofauti ni mkubwa kwa sababu sisi tunatoa huduma zetu kwa kushirikiana moja kwa moja na makampuni na wafanyabiashara wakubwa na wanaoaminiwa nchini na duniani kwa ujumla. Hivyo hofu ya wateja kununua bidhaa feki, sio halisi na zilizo chini ya kiwango halipo kwa upande wetu. Kwa mfano; Tigo, Tecno, Samsung, Apple, Sony, Philips, Hp, Delly, Lenovo, LG, Hitachi, Tronic, Kenwood, Bruhm, Revlon, Epson, Hisense, Panasonic, kampuni hizi zote yaliyopo kwenye mtandao wetu yanasifika kwa ubora na uhalisi wa bidhaa zao duniani,” aliongezea Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania.

Ikiwa inaadhimisha miaka sita ya kuleta mapinduzi ya huduma za manunuzi ya mtandaoni Afrika, Jumia imefanikiwa kuwashawishi wafanyabiashara na wateja wengi kuamini na kuhamia kwenye mfumo huu mpya.

“Tunafahamu sio kazi rahisi kuwaaminisha watanzania wote kuwa manunuzi ya mtandaoni ni salama na rahisi kama wanavyokwenda dukani. Katika kuhakikisha tunafanikiwa kuwashawishi na kuwazoesha taratibu, Jumia inafanya shughuli zake kulingana na matakwa ya wateja,” alisema na kumalizia Bw. James kuwa, “Kupitia mtandao wetu pekee mteja anaweza kuagiza huduma kwa gharama nafuu, akapelekewa mpaka mahali alipo, akaikagua bidhaa baada ya kujiridhisha ndipo hufanya malipo. Kama hiyo haitoshi, tunayo sera ya kurudisha bidhaa bure bila ya malipo yoyote endapo mteja ameletewa bidhaa ambayo hajaridhika nayo, kitu ambacho hutokea mara chache sana kutokana na umakini wa timu yetu.”

Kuhusu Jumia
Jumia ni mtandao wa unaongoza kwa uuzaji na manunuzi ya bidhaa barani Afrika.
Jumia inalenga kutengeneza mustakabali wa mazingira mazuri ya masoko na sehemu ya kununua na kuuza bidhaa, pamoja na huduma za kimtandao na kifedha.

Jumia inajenga miundombinu ya biashara Afrika kwa ajili ya vizazi vijavyo kupitia mtandaoni na masoko yenye hadhi ya juu mahali popote, ikitoa huduma nafuu na rahisi kwa wateja na kuwasaidia kutimiza mahitaji yao ya kila siku. Dhamira ya Jumia ni kubadili na kuboresha maisha ya watu kupitia teknolojia.

Kupitia majukwaa na huduma zake tofauti kama vile Jumia eCommerece, Jumia Travel, Jumia Food, Jumia House, Jumia Deals, Jumia Jobs, Jumia Pay, na Jumia One, Jumia inachochea ukuaji uchumi wa bara la Afrika kupitia mabadiliko ya kidigitali. Jumia inaunga mkono ukuaji wa makampuni ya Kiafrika na kuyapatia wigo mkubwa mpana zaidi. Zaidi ya makampuni 50,000 yenye asili ya Afrika na watu binafsi wanafanya biashara kupitia Jumia.

Ikiwa inawezeshwa na wafanyakazi takribani 3,000, Jumia imejizatiti katika mustakabali wa bara la Afrika. Jumia inatengeneza fursa za ajira na kufungua milango kwa waafrika wenye vipaji kujipatia na kuendeleza ujuzi mpya.

Jumia ilianzishwa mwaka 2012 na kujitanua kwenye nchi takribani 13 (ikiwemo Afrika ya Kusini kupitia Zando, mtandao wa mitindo ya mavazi). Inaungwa mkono na wadau kama vile: MTN, Millicom, Rocket Internet, Axa, Orange, Goldman Sachs na CDC Group.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.