Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Dotto James akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Profesa Raphael Chibunda wapili kutoka (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Maendeleo la Taifa NDC Profesa Damian Gabagambi wakwanza (kulia), Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wapili kutoka (kulia),
akikata utepe kuzindua Matrekta 10 ambayo ameyakabidhi kwa Chuo hicho cha SUA
kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei
2018.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Dotto James akipunga mkono pamoja na viongozi wengine mara baada ya
kuzindua na kuyakabidhi Matrekta hayo 10 kwa Chuo cha SUA katika hafla fupi
iliyofanyika katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta hayo cha URSUS- TAMCO
Kibaha mkoani Pwani.
Sehemu ya Matrekta 10
yaliyokabidhiwa leo kwa Chuo cha SUA ikiwa ni
utekelezwaji wa ahadi ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipotembelea
chuo hicho mkoani Morogoro tarehe 7 Mei 2018.
No comments:
Post a Comment