Habari za Punde

MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUYUNGU YAKAMILIKA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WAPIGWA MSASA.

 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko Lusubilo, Kigoma Bw. Joeli Mwakibibi akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura leo (11 Agosti 2018) wakati wa mafunzo ya Kusimamia uchaguzi  mdogo wa Ubunge utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Uchaguzi katika jimbo la Buyungu (hawapo pichani), wilayani Kakonko wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kusimamia Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo leo 
 Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kiziguzigu Bi. Jesca Masawe akifafanua jambo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura wakati wa mafunzo ya kusimamia uchaguzi mdogo katika jimbo la Buyungu leo.
 Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ya Kakonko  Bi. Martina Ulungi akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kufunga lakiri (seal) za usalama kwenye maboksi ya kura wakati wa mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura leo wilayani Kakonko.
Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura wakati wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kusimamia uchaguzi mdogo katika jimbo la Buyungu leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.