Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman Afanya Uteuzi wa Masheha

Mkuu wa Mkoa wa 
Kusini Pemba Mh. 
Hemed Suleiman 
Abdulla amefanya 
uteuzi wa Masheha 
saba katika shehia 
mbalimbali za Wilaya 
ya Mkoani na Chake 
Chake.
Mkuu huyo wa Mkoa 
amefanya uteuzi huo 
kwa mujibu wa 
kifungu cha 8(10) cha Sheria Namba 8 ya mwaka 2014, 
Sheria ya Tawala za Mikoa Zanzibar.
Katika Wilaya ya Chake Chake walioteuliwa ni Haji 
Mohammed Ali wa Shehia ya Wesha, Khamis Suleiman Ali 
wa Shehia ya Kwale na Abrahman Shehe Moh’d wa Shehia ya 
Chachani.

Katika Wilaya ya Mkoani walioteuliwa ni Simai Faki Simai 
wa Shehia ya Mkungu na Sheria Makame Haji wa Shehia ya 
Makombeni.

Wengine ni Omar Bakar Omar wa Shehia ya Kukuu na 
Afadhali Juma Afadhali wa Shehia ya Kangani.
Uteuzi huo umeanza leo Agost 7.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 07.08.2018

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.