Habari za Punde

Mhe Aweso Amlilia Rais Magufuli Ujenzi wa Barabara ya Tanga Pangani na Saadan.

 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni mjini Pangani ambako pamoja na mambo mengine aliweza kusikiliza kero zao zinazowakabili
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni mjini Pangani ambako pamoja na mambo mengine aliweza kusikiliza kero zao zinazowakabili
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani akizungumza katika mkutano huo
  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akiwa amebebwa juu na wananchi mara baada ya kumaliza kuwahutubia
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa Abdallah wakifuatilia hoja za wananchi kwenye mkutano huo
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa Abdallah akimtunza msaanii Dkt Nyau
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akimtunza mmoja wa wananchi
sehemu ya wananchi wa mji wa Pangani wakimfuatilia  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
Wananchi wakimfuatilia  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)


Na.Assenga Oscar
SERIKALI ya awamu ya tano imeombwa kuangalia namna ya kuanza ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani, Saadan hadi Bagamoyo ili kuweza kumaliza kilio cha wananchi wa wilaya ya Pangani cha muda mrefu ikiwemo kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa mkoa .

Ombi hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara wilayani humo ambapo alisema pamoja na kuwepo kwa miradi mingi inayotekelezwa huko lakini kilio kikubwa cha wananchi wake ni ukosefu wa barabara nzuri.

Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) alisema wakati Rais Magufuli akiomba kura kwa wananchi hao mwaka 2015 aliwaahidi wananchi ujenzi wa barabara hiyo na walikubali kumpa kura nyingi na imani kubwa kwake kwa mategemeo ya kumpata mkombozi atakae weza kumaliza kero hiyo ambayo imedumu katika awamu zote nne zilizopita bila ya mafanikio.

“Kwenye mkutano wangu wa leo hii nipo hapa nyumbani kama Mbunge wenu kawaida na sikuja kama Naibu Waziri na jukumu la Mbunge ni kuwasemea wananchi wake Mh Rais wananchi wangu kiukweli wanalia na suala la barabara hii na hawajui hatma yake lini mradi huu utaanza”Alisema Aweso.

Hata hivyo alisema kuzorota kwa uchumi na maisha magumu kwa wananchi wa wilaya hiyo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la kutokujengwa barabara ambayo ingesaidia kufungua wilaya hiyo ambayo inaonekana kama
imesahaulika katika nyanja zote.

Hata hivyo akionyesha kuunga mkono ujenzi wa barabara hiyo Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella alimueleza Waziri wa Fedha na Mipango Phillip Mpango juu ya umuhimu wa barabara ya Tanga, Pangani hadi Saadan wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Kiislam ya Amana

“Mh kilio kikubwa ni tatizo la barabara ya Tanga –Pangani Saadani tunaomba mtusaidie suala hilo kwani hakuna ukombozi unatarajiwa na wananchi wengi mkoani Tanga zaidi ya ujenzi wake”Alisema.

Shigella alimueleza hadharani Waziri huyo wa fedha kuwa Serikali inapaswa kufanya kila njia kuhakikisha inatenga fedha za kutosha ili kukamilisha mradi huo ambao bado hatma yake haijulikani utaanza lini.

Alisema Tanga ni Mkoa ambao unafunguka kiuchumi hasa katika swala zima la viwanda na matarajio ya barabara hiyo inaweza kurahisisha shughuli mbalimbali za kibiashara, usafirishaji wa mazao na utalii katika Mbuga ya Saadan hivyo ni jukumu la Serikali kuhakikisha barabara hiyo
inajengwa.

“Waziri wa fedha tunaomba mchako wa fedha kwa ajili ya barabara hiyo ufanyike kwa wakati ili kuwakomboa wananchi wa maeneo hayo na kukuza pato la Mkoa,Wilaya na hata mtu mmoja mmoja”Alisema Shigella.

Awali akizungumzia suala la ujenzi wa barabara hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philp Mpango alisema wamiliki wa viwanda,wafanyabiashara wakubwa na wadogowadogo wajitahidi kulipa kodi ili fedha hizo ziweze kujenga miundombinu ndani ya Nchi.

Alisema Serikali kupitia ukusanyaji wa kodi zake inahakikisha inatenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukatabati wa miundombinu ili kuondoa kerokwa wananchi katika maeneo husika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.