Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali. Mohamed Shein Amefanya Uteuzi wa Viongozi leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohmed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Wizara ya Elimu na Mafuno ya Amali na Wizara ya Afya kama ifuatavyo:

1. UTEUZI WA OFISA MDHAMINI WA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI – PEMBA.

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, na kifungu cha 12(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Mohamed Nassor Salim kuwa Ofisa Mdhamini  katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali - Pemba. 

Bwana Mohamed Nassor Salim anachukua nafasi ya Bwana Salum Kitwana Sururu ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale katika Wizara Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

2. MKURUGENZI WA IDARA YA TIBA KATIKA WIZARA YA AFYA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, na Kifungu cha 12(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Dkt. Juma Salum Mbwana kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba katika Wizara ya Afya.

Dkt. Juma Salum Mbwana anachukua nafasi ya Dkt. Mohamed J. Dahoma ambaye atapangiwa kazi nyengine. Uteuzi huo umeanza leo tarehe 13 Agosti 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.