Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akipata maelezo mbalimbali
kutoka kwa Afisa Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Edward Kimaro alipotembelea banda la Maonesho ya Kilimo na sherehe
za Nanenane la Mamlaka, yanafanyika kwenye Uwanja wa Nyakabidni mkoani Simiyu.
Raia wa China wanaofundisha kwenye shule
ya ya sekondari ya J.W.Bukanga Musoma, Bi. Jane Lee (wapili kushoto) na Bi. Cary Zhang (watatu kushoto) wakimsikiliza
Afisa Usalama Mwandamizi wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Bakari Mwalwisi alipokuwa akitoa maelezo kuhusu vimiminika kwenye banda la
maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye
Uwanja wa Nyakabindi, mkoani Simiyu.
Na
Mwandishi Wetu, Simiyu
SHIRIKA
la Mawasiliano nchini (TTCL), limeahidi kutoa
gawio kubwa zaidi kwa serikali mwakani,
ili fedha hizo
zikasaidie katika kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa
miundombinu
ya viwanja vya ndege vya serikali.
Hata
hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri
Kindamba ambaye alitembelea banda la
maonesho ya Kilimo
la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
yanayofanyika
kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani
Simiyu, amesema wingi huo wa fedha utatokana
na
mashirika na taasisi za umma kuwaunga mkono kwa
kutumia huduma mbalimbali
zinazotolewa na shirika hilo.
“Mwaka
huu tulitoa gawio la sh. Bil 5.1 kwa serikali, lakini
ninaimani mwakani tutatoa
zaidi endapo tutapata
ushirikiano wa kutumiwa kwa huduma zetu kutoka kwenye
taasisi nyingine za serikali, ambapo fedha
hizo zinasambazwa na serikali kwenye
kazi mbalimbali
ukiwemo wa ujenzi wa viwanja vya ndege,” amesema Bw.
Kindamba.
Bw.
Kindamba ameishukuru TAA kwa kuanza kutumia
huduma ya mawasiliano ya simu kutoka
kwenye shirika hilo,
ambapo itasaidia kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi.
Amesema
anaahidi kuimarisha ushirikiano na TAA, na wapo
tayari kutumia huduma zinazotolewa
na mamlaka kwa
maslahi ya nchini, ili kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi.
“Ushirikiano
wetu utasaidia kuongeza mapato, ambapo kila
taasisi moja itaweza kutumia huduma
na bidhaa za taasisi
nyingine, kwa lengo la kuzifanya ziendelee kukua na
kuimarika kiuchumi, kwani taasisi za umma zinategemeana
zenyewe kwa zenyewe,”
amesema.
Pia
ameipongeza TAA kwa jitihada zake za kujitangaza kwa
wananchi, ambapo ameitaka
kuendelea kuboresha
miundombinu ya viwanja vya ndege.
“Nawapongeza
kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kujitangaza,
naomba muendelee kuboresha viwanja
vya ndege kwa
maslahi ya Watanzania wote, kwa kweli najivunia sana
uwepo wenu
katika Nanenane “I am proud of your success’
na kweli mna iunganisha Tanzania
kwa Ulimwengu,”
amesema Bw. Kindamba.
No comments:
Post a Comment