Habari za Punde

Ujio wa Ujumbe wa Indonesia kuleta neema ya maendeleo ya kuchumi na kijamii

Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Salum Muhammed amesema ujio wa Ujumbe wa Serikali ya Indonesia hapa nchini umeleta matumaini ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Vuga alipokuwa akizungumza na ujumbe huo na kusema mashirikiano yalioanzishwa katika ya ncghi hizo mbili yataweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika nchi hizo.
Amesema lengo la kufanya ziara hiyo kuangalia fursa zilizopo na kufanya mazungumzo na Wataalamu wa Zanzibar ili kuweza kuangalia miradi ya kiuchumi itakayoweza kuleta maendeleo katika nchi hizo mbili.
Amesema Ujumbe huo utaweza kuangalia zaidi fursa za viwanda zinavyotokana na Bahari kuu,Usafiri wa Bahari kuu na Utalii.
Hata hivyo amesema Ujumbe huo umefurahia mazingira ya Zanzibar na kuwepo kwa amani na utulivu na kusema wapo tayari kushirikiana na Zanzibar katika mambo yatakayoweza kuleta manufaa katika nchi hiyo kwa kuanza ujenzi wa Miondombinu ya kuhifadhia mafuta katika eneo lilopangwa la Mangapwani.
Nae kiongozi wa Msafara huo kutoka Serikali ya Indonesia Daniel Simanjuntak amewpongeza Viongozi wa Zanzibar kwa kukubali kwa dhati kuanzisha mashirikiano yatakaweza kuleta maendeleo katika Nchi mbili hizo.
   Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.