Habari za Punde

Wasifu wa John McCain

Senator John McCain
John McCain alikuwa ni shujaa wa vita vya Vietnam ambaye alikuwa mwanasiasa aliyeheshimika sana nchini Marekani.
Ni mwanasiasa mwenye msimamo mkali ambaye mara nyinyi alikuwa anatofautiana na wanachama wenzake wa Republican na alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wake Rais Donald Trump
Alishindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2008 huku akilaumiwa kwa uamuzi aliofanya wa kumteua Gavana wa Alaska Sara Palin kuwa mgombea mwenza.
Baba yake na babu wote walikuwa ni wanajeshi.
John Sidney McCain III Alizaliwa Agosti 29 mwaka 1936 kwenye kambi ya jeshi huko Coco Solo panama, eneo ambalo wakati huo lilikuwa chini ya udhibiti wa Marekani. Taaluma ya kijenshi ilikuwa tayari kwenye damu yake kwa sanbabu baba yake na babu wote walihumu kama wanajeshi na hata wakashika nyadhifa za juu.
Mwana wa afisa mwandamizi katika jeshi la majini, Bw McCain alihitimu kutoka chuo cha jeshi la majini mwaka 1958 na alianza kazi ya urubani wa jeshi akiwa na umri wa miaka 22.
Akapelekwa vitani nchini Vietnam, alinusurika kifo Julai ya mwaka 1967, wakati alipokuwa akijiandaa kwenda kufanya shambulio la anga, kombora liligonga matanki ya mafuta, hali iliyosababisha moto kwenye meli na watu 134 walipoteza maisha.
McCain (kulia) akiangalia uharibifu kwenye meli ya USS Forrestal mwaka 1967.
Miezi mitatu baadaye alitunguliwa kaskazini mwa Vietnam. Akakamatwa na wapiganaji wa Vietnam, alikataa kuachiliwa mapema.
Badala yake, alishikiliwa kama mfungwa wa kivita kwa zaidi ya miaka mitano, mahali alikokuwa akipigwa mara kwa mara na kuteswa hali iliyosababisha matatizo katika mikono yake.
Baada ya kurejea Marekani aliendelea kutumikia jeshi, hatimaye akawa mwambata wa jeshi la majini kwenye baraza la Seneti mpaka aliposataafu mwaka 1981.
Wanajeshi wa Vietnam Kaskazini wakimtoa majini baada ya ndege yake kudunguliwa.
Baada ya kuachiliwa alikaribishwa nyumbani na Rais Nixon

Maisha ya kisiasa.

Ilikuwa ni wakati huu ndipo alipohamia Arizona kujijenga katika maisha ya kisiasa, alifanikiwa kushinda uchaguzi wa Seneti mwaka 1982.

Akigombea dhidi ya George W Bush mwaka 2000 kuwania uteuzi wa chama cha Republican, Bw McCain awali alipata kuungwa mkono na kufanikiwa kushinda kura za maoni katika jimbo la New Hampshire.
Lakini alikabiliwa na upinzani mkali, akishambuliwa katika kampeni kwa kuchafuliwa, na hatimaye akahitilafiana na wajumbe wenye ushawishi mkubwa ndani ya chama wanaoegemea zaidi kwenye dini.
Alilizimika kuondoka kwenye uteuzi wa kuwania urais katika chama cha Republican mwaka 200.
Bw Bush alisonga mbele kwa kushinda uteuzi wa chama cha Republican na McCain akarejea kwenye baraza la Seneti, akitumikia katika kamati muhimu ya maswala ya jeshi.
Bw McCain tangu wakati huo ameongeza msimamo mkali kuhusu baadhi ya maoni yake kama utoaji mimba, lakini bado haiminiki kikamilifu miongoni mwa wainjilisti kuwa yeye anafuata misingi ya kidini kama wao.
Licha ya kuahidi kumuunga mkono Bush, alionyesha wazi kuwa hakuwa na hofu ya kumkosoa rais mpya. Alikuwa mmoja wa maseneta wawili wa Republican waliopiga kura kupinga kupunguzwa kodi na kuping sera za rais kuhusu kudhibiti bunduki.
Baada ya mashmbulizi ya Septemba 11 aliunga mkono vita vya George Bush nchini Afghanistan, lakini baadaye aliweza kuhoji kuhusu mikakati ya Bush na sera za waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld.

Matokeo mabaya

Mwezi Aprili mwaka 2005 McCain tena alitangaza kuwa angewania uraia ambapo alipambana na washindani wawili kutoka kwa meya wa Nee York Rudy Giulani na meya wa Massachusetts Mitt Romney katika uteuzi wa Republican.
Hata hivyo alishangaza kila mtu kwa kumteu mwanasiasa asiye na umaarufu Sarah Palin gavana wa Alaska kama mgombea mweza.
McCain na Sarah Palin.
Wapiga kura walianza kutilia shaka hali yake ya kutokuwa na ujuzi na matokeo mabaya kwenye mijadala na televisheni hali iliyoyumbisha kampeni ya chama cha Republican.
Kwa kushindwa katika matumuzi, McCain alishindwa, na Obama akaingia Ikulu.
McCxaina akiwasili bungeni Juni 27 mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.