Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba Aweka Jiwe la Msingi Skuli ya Maandalizi Kizimkazi Mkunguni na Kuahidi Kuchangia Mifuko 50 ya Saruji na Mabati 50. Ili kumalizia Madarasa Hayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba akisalimiana na Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi Kizimkazi Mkunguni wakati alipofika kuweka Jiwe la Msingi la Jengo hilo jipya likiwa na madarasa manne, akiwa katika ziara yake katika Kijiji cha Kizimkazi kuhudhuria Siku ya Kizimkazi Day inayotarajiwa kufanyika kesho katika Kijiji hicho Mkoa wa Kusini Unguja na Mgeni Rasmin anategemewa kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

Jengo Jipya la Skuli ya Maandalizi kwa Watoto wa Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni lililojengwa kwa nguvu za Wananchi wa Kizimkazi kwa ajili ya kutowa Elimu ya Maandalizi kwa Watoto wao wanaojiendaa kuaza darasa la kwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba akiondoa kipazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo hilo jipya la Skuli ya Maandalizi kwa Watoto wa Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya jengo hilo katika Skuli ya Sekondari Kizimkazi Mkunguzi Mkoa wa Kusini Unguja. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba akipiga makofi kuashiria kusherehekea uzinduzi huo baada ya kuondoa kipazia cha jiwe la msingi la jengo jipya la Skuli ya Maandalizi Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa katika ziara yake kutembelea kijiji hicho kuhudhuria sherehe za Siku ya Kizimkazi Day zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Shehia ya Kizimkazi Mkunguni Mzee Hassan Mkadam akitowa maelezo ya ujenzi huo, kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo lao jipya la Skuli ya Maandali ya Watoto kujiandaa na kuaza darasa la kwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba akizungumza na kutowa shukrani kwa Wananchi kushirikiana na kufanikisha ujenzi wa jengo hilo kwa ajili ya kutowa Elimu ya Maandalizi ya Watoto wao na kutoa ahadi ya kuchangia mifuko 50 ya saruji na mabati 50 kufanikisha ujenzi huo ili kuweza kutowa huduma ya Elimu kwa Watoto hao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba akiangana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Shehia ya Kizimkazi Mkunguzi Mzee Hassan Mkadam, baada ya kumaliza hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo huko kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.  
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Yussuf Makamba akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali walioshuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo Jipya la Madarasa Mane ya Skuli ya Maandalizi Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja lililojengwa kwa nguvu za Wananchi wa Kijiji hicho.Kwa kushirikiana na Viongozi wao Mbunge na Mwakilishi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.