Habari za Punde

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga Ampa Kibarua Mkurugenzi wa Ramani Kutatua Migogoro ya Mipaka Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati alipokuwa kawasili katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro katika ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na wananchi wa vijiji viwili vya Katekate na Iputi kwa ajili ya kutatua mgogoro katika ya vijiji hivyo na  Pori la Akiba la Selous .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati alipokuwa kawasili katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro katika ziara yake ya kikazi ya kuzungumza na wananchi wa vijiji viwili vya Katekate na Iputi kwa ajili ya kutatua mgogoro katika ya vijiji hivyo na  Pori la Akiba la Selous .
Mbunge wa jimbo Ulanga, Gudluck Milinga akizungumza na wananchi wa Katekate akimweleza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kuhusu mgogoro wa mipaka katika eneo linalogambaniwa na wanakijiji hicho na  Pori la Akiba la Selous.
Kaimu Katibu Tawala, Huluka Hamisi akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Iputi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kuzungumza na wanakijiji cha Iputi kwenye mkutanao wa hadhara uliofanyika jana 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa eneo   linalogombaniwa kati ya wanakijiji wa Katekate na Pori la Akiba la Selous ambapo  eneo hilo linasemekana kuwa  sio eneo la  hifadhi wala si eneo la  wanakijiji ambapo kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo  amesema litatumika kwa ajili ya kuanzisha Jumuiya ya wanyamapori ambapo wanakijiji hao ndo watakuwa wanufaika namba moja kama Mkurugenzi wa Ramani atabaini kuwa si eneo la Hifadhi wala la wanakijiji wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kijiji cha Katekate wilayani Ulanga mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi wa  Kijiji cha Katekate wakifutilia mkutano wa hadhara wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alipokuwa akizungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa eneo   linalogombaniwa  kati ya wanakijiji wa Katekate na Pori la Akiba la Selous.

 ((Picha zote na Lusungu Helela-MNRT)


Na.Lusungu Helela - Morogoro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewasihi wananchi wa vijiiji vya Iputi na Katekate wilayani Ulanga mkoani Morogoro wawe  wavumilivu wakati wanasubili wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoka  ofisi ya Mkurugenzi wa ramani kuja  kusoma ramani ili kuweza kubaini mipaka halisi ya baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba la Selous.

Amesema  migogoro ya mipaka kati ya Selous  na  vijijji hivyo hakuna mwenye dhamana ya kuonesha mipaka hiyo  kwa vile wote ni wanaufaika, Hivyo lazima kuwepo na mtu wa upande wa tatu wa kuamua ambaye ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

‘’ Selous wanatamani wawe na eneo kubwa zaidi kwa ajili ya wanayamapori vivyo hivyo Wanavijiji nao wanatamani wawe na eneo kubwa zaidI ajili ya shughuli za kilimo hivyo hakuna atakayeshinda’’ alisema Waziri Hasunga

Amesema hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mipaka inapowekwa kwenye Hifadhi lazima wawepo viongozi  wa Vijiji, baadhi ya wazee wa vijiji pamoja na uongozi wa wilaya wakishuhudia uwekaji wa mipaka hiyo ukifanywa na Wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Ramani.

Rai hiyo imetolewa jana wilayani Ulanga mkoani Morogoro wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kwa nyakati tofauti na Wananchi wa vijiji vya Iputi na Katekate wakimlalamikia kuwa          mipaka katika vijiji vyao  imewekwa pasipo kuwashilikisha hali iliyopelekea maeneo yao makubwa kuchukuliwa na Pori hilo.

Awali, Mbunge wa jimbo  la Ulanga, Gudluck Milinga amemueleza Naibu Waziri Hasunga kuwa  mipaka ya maeneo ya vijiji hivyo imekuwa ikihamishwa hamishwa hali inayopelekea kuleta manung’uniko kutoka wananchi wake.

Ameongeza kuwa kutokana na  ubadilishaji  badilishaji mipaka hiyo  unaofanywa na Pori hilo  imesababisha  wananchi  wa vijiji hivyo kutokuwa na mahusiano mazuri na hifadhi hiyo.

Aidha, Mbunge huyo amemuomba Naibu Waziri Hasunga aweze kuingilia kati mgogoro huo hasa mgogoro katika  kijiji cha  Katekate ambapo kuna eneo linalogombaniwa  kati ya wanakijiji na Pori Akiba la Selous na kwa mujibu wa maelezo  eneo hilo sio la hifadhi wala la wanakijiji.

Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri huyo amemhakikishia kuwa mara baada ya watalaam watakapokuja kusoma ramani ili kubaini eneo hilo endapo itaonekana kuwa halina mwenyewe basi litatumiwa na wanakijiji hao kwa ajili ya kuanzisha Jumuiya ya wanyamapori (WMA) ambapo wanakijiji hao ndo watakuwa wanufaika namba moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.