Habari za Punde

Bado kuna mwamko mdogo katika jamii kuwapeleka watoto Skuli

Na Takdir Ali,                                         1-09-2018.
Kiasi ya Watoto laki tatu na elfu 40 wenye umri wa kusoma wako nje ya madarasa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mwamko mdogo wa Wazazi na Walezi wa kuwapeleka Skuli.
Kwa mujibu wa utafiti uliofadhiliwa na UNICEF, na Zanzibar Milele Foundation mwaka 2016 umeonyesha kuwa idadi hiyo imesababishwa na Umasikini,Wanafunzi kuadhibiwa na kufuata huduma elimu masafa ya mbali.
Akifunga Semina ya siku 3 kwa wajumbe wa kamti za mashauriano katika shehia za wilaya ya Magharib B, Mkurugenzi wa Kituo Makuzi na Maendeleo ya mtoto ya madras,Mwalim Khamis Abdallah Saidi amesema baada ya kubaini hali hiyo wameanzisha mradi wa ushawishi wa elimu katika Wilaya hiyo.
Amefafanua kuwa lengo la mradi huo wnaouendesha kwa kushirikiana na Wizara ya elimu na Zanzibar Milele Foundation ni kupita na kuhamasisha nyumba hadi nyumba ili watoto waweze kupelekwa au kurudishwa Skuli.
Hata hivyo Mwalim Khamisi amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao skuli wakiwa na umri sahihi kwa lengo la kuweza kupata kujua kuandika, kusoma na kuhesabu.
Nae Mratibu wa Mradi wa Mradi huo Safia Salum Muhammed amesema baada ya  kumalizika Mradi huo wanategemea kuongeza uandikishaji wa watoto katika madarasa ya maandali na msingi wakiwa na umri sahihi kwani inaonekana asilimia kumi na saba ya watoto wanaoandikishwa Wilaya  Magharibi B wanaumri mkubwa.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.