Habari za Punde

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Awataja Wananchi Waliopta Ajali Juzi Dunga.

Watu wawili wamefariki na wawili kujeruhiwa katika ajali ya gari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan Suleiman alisema tukio hilo limetokea jana  Agust 31 , majira ya saa 11.20 asubuhi.

Gari hiyo aina ya VITZ yenye namba za usajili Z.815 JM, iliyokuwa ikitokea upande wa Mchangani shamba kuelekea Kidimni ilipofika maeneo ya Dunga mitini  iliacha njia na kugonga jengo la kituo cha Petroli.

‘Ndani ya gari hiyo kulikuwa na watu wanne, ambao wawili walikuwa siti ya nyuma na wawili mbele, akiwemo dereva ambae amefariki kutokana na gari hiyo  kuwaka moto”, alisema.

Kamanda Suleiman aliwataja waliofariki kuwa ni Mohammed Fahad Mohammed (22) mkaazi wa kiembesamaki, na mwengine ni Mudathir Othman Ibrahim (23), mkaazi wa Shangani Mjini Unguja.

Kamanda huyo alisema amjeruhi waliokuwa ndnai ya gari hiyo ni Ahmed Sleiyum Mbarouk (22) mkaazi wa Kiembesamaki na mwengine Sofia Ali Mohammed (20) mkaazi wa Mtendeni Mjini Unguja.

Alisema majeruhi walikaa siti ya nyuma hivyo, waliwahi kufungua mlango na kushuka. majeruhi hao walifikishwa katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja na kupatiwa matibabu ambao Sofia aliruhusiwa na Ahmed bado anaendelea na matibabu.

Kamanda huyo alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari, hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka madereva kuacha kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi na kusababiha kutokea  kwa ajali zizokuwa za lazima.

Jeshi la Polisi Mkoa huo linaendelea na upelelezi wa ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.