Habari za Punde

CHANGAMOTO YA KUPUNGUA KWA MAJI MTO MARA KUPATIWA UFUMBUZI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akiwa amesimama pemebezoni mwa Mto Mara eneo la ‘Kogatendo’ na kupata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Serengeti Bw. William Mwakilema juu ya kupungua kwa maji katika Mto huo. Waziri Makamba ameahidi kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo mapema iwezekanavyo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akiwa amesimama pemebezoni mwa Mto Mara eneo la ‘Kogatendo’ na kupata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Serengeti Bw. William Mwakilema juu ya kupungua kwa maji katika Mto huo. Waziri Makamba ameahidi kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo mapema iwezekanavyo.


Bw. William Mwakilema (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba mara baada ya kutembelea Mto Mara eneo maalumu ambalo wanyama aina ya nyumbu huvuka kwa makundi na kuwa kivutio kikubwa cha utalii.


Eneo la Kogatendo katika Mto Mara ni miongoni mwa maeneo ambayo wanyama aina ya nyumbu huvuka kwa makundi na kuwa kivutio cha utalii. Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira January Makamba ametembelea eneo hilo ili kuhakikisha hatua zinachukuliwa kurejesha ikolojia ya mto huo katika hali ya awali.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na 

Mazingira Mhe. January Makamba amewakumbusha 

watendaji wa Wilaya ya Serengeti wajibu wao wa kipekee wa 

ulinzi katika hifadhi ya mbuga ya Serengeti kwakuwa Wilaya 

yao imebeba jina linalojulikana duniani kote ikiwa ni pamoja 

na eneo maalumu la wanyama aina ya Nyumbu ambao 

huvuka kwenda upande wa pili na kuwa miongoni mwa 

vivutio vikubwa vya utalii.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo Wilayani Serengeti 

mara baada ya kufanya ziara ya kikazi Wilayani hapo 

kujionea uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira na kutembelea 

eneo la mto Mara eneo ambalo ni muhimu sana ki-ikolojia.

Katika kikao na viongozi wa Wilaya hiyo, Mhifadhi Mkuu wa 

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Bw. Wiliam Mwakilema 

aliainisha kuwa mtiririko wa maji katika Mto Mara kutoka 

chanzo chake kikuu katika Milima ya Mau nchini Kenya 

kimepungua kutokana na shughuli za kibinadamu na 

matumizi mengine yasiyoendelevu jambo linalohatarisha 

kupungua kwa mtiririko wa maji katika Mto Mara kwa 

kipindi kirefu, eneo ambalo ni kivutio pekee cha wanyama 

wanaohama dunia.

Katika kutatua tatizo hilo Waziri Makamba amesema kuwa 

masuala ya mazingira ni mtambuka hivyo Ofisi yake yenye 

dhamana na kusimamia hifadhi ya Mazingira nchini itafanya 

ziara ya kikazi nchini Kenya kwa lengo la kujadiliana na 

kupata ufumbuzi wa haraka juu ya jambo hilo.

“Sisi na wenzetu wa Kenya tumeingia mkataba mwaka 2013 
wa matumizi sahihi ya rasilimali katika Mto Mara na kutunza ikolojia yake, kwa kushirikiana na Mawaziri wenzangu wa Maji na Maliasili na Utalii, tutafanya ziara nchini Kenya ili kwapamoja tupate ufumbuzi wa jambo hili ikiwa ni pamoja na Ziwa Chala, Ziwa Jipe na Ziwa Natroni ambayo yote yako pande mbili yaani Tanzania na Kenya.”

Waziri Makamba amesema Serikali itahakikisha maslahi ya 

Nchi yanalindwa kwa njia za ki-diplomasia na kuhakikisha 

Mto Mara unatiririsha maji kipindi chote cha mwaka.

Waziri Makamba amehitisha ziara yake Mkoani Mara na 

amewasili Mkoani Arusha ambapo atakuwa na vikao wa 

wadau wa hoteli mbalimbali na kambi za uwindaji kwa lengo 

la kuweka mikakati ya kuhifadhi mazingira maeneo ya 

mbugani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.