Habari za Punde

Jose Mourinho: Mkufunzi wa Man Utd Asema Kwamba Yeye Bado ni Mmoja wa Kocha Bora Zaidi Duniani

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atakuwa mmojawapo wa wakufunzi bora zaidi duniani hata iwapo hatposhinda ligi ya Uingereza na klabu hiyo.
United imepoteza mewchi mbili kati ya tatu iliocheza , ikiwa ni mwanzpo mbauya tangu mwaka 1992-93.
Akitetea rekodi yake , mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 55 alisema kuwa ndio meneja wa pekee kushinda mataji ya ligi akiwa Itali, Uhispania na Uingereza.
Pia amesema kuwa kuma;liza katika nafasi ya pili katika ligi hiyo ni mojwapo ya ufanisi mkubwa. Alipoulizwa iwapo atakuwa miongoni mwa wakufunzi bora iwapo hatoshinda taji la ligi ya Uingereza na man United , alijibu ndio.
Mourinho amejitetea kuhusu kazi yake siku chache tu baada ya timu yake kulazwa 3-0 na Tottenhama katika uwanja wa Old Trafford.-ikiwa ndio matokeo mabaya zaidi ya nyumbani katika ukufunzi wa Mourinho.
Alitawataka waandishi habari kumuheshimu , na kuwakumbusha kwamba mataji mataytu ya ligi ya Uingereza alioshinda awali na Chelsea ni zaidi ya wakufunzi wote walioshinda wakiwa Uingereza.
kabla ya mechi yake dhidi ya Burnley siku ya Jumapili, raia huyo wa Ureno aliongeza: Nilifanikiwa pakubwa msimu uliopita na hilo ndio swala ambalo hamtaki kulkubali.
Misimu miwili iliopita tulikuwa na msimu mzuri ka sababu tulishinda taji la Yuropa. Tulishinda kwa sababu lilikuwa katika viwango vyetu. man United ndio timu ya mwisho Uingereza kushinda taji la Yuropa.
Mimi ndio meneja wa pekee kushinda mataji manane Italy, Uhispania na Uingereza-sio mataji madogo-na kuibuka wa pili msimu uliopita ni miongoni mwa ufanisi mkubwa niliopata.
Wakati Mourinho alipoambiwa kwamba mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alikabiliwa na maswali kama hayo msimu uliopita, Mourinho alijibu: kwa sababu hakushinda chochote katika soka ya kimataifa.
"Hilo ni tataizo lake , ninawaambia kile ninachofikiria, na vile ninavyohisi. Na ninajibu swali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.