Habari za Punde

Kamati ya Fedha biashara na Kilimo ya baraza la wawakilishi ziarani Pemba

KAIMU mkurugenzi mkaazi wa Mamlaka ya Ukuzaji wa Vitega Uchumi Zanzibar Tawi la Pemba, Ali Shaaban Suleiman akionyesha wajumbe wa kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la wawakilishi,  mipaka ya Maeneo huru ya Uwekezaji Micheweni eneo ambalo limetekwa kwa maazi lenye ukubwa wa Hekta 261.4, wajumbe waho walipotembelea maeneo hayo.(PICHA NA ABDI ZULEIMAN, PEMBA)

AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba, Ibrahim Saleh Juma akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Fedha biashara na Kilimo ya baraza la wawakilishi, wakati walipotembelea maeneo huru ya uwekezaji vitega uchumi Micheweni.(PICHA NA ABDI ZULEIMAN, PEMBA)
 MWENYEKITI wa Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt Mwinyihaji Makame Mwadini akisikiliza kwa makini maelezo mafupi yaliyosomwa na Mkurugenzi Mkaazi wa ZIPA Pemba, Ali Shaaba Suleiman juu ya maeneo huru ya uwekezaji Micheweni.(PICHA NA ABDI ZULEIMAN, PEMBA)
MWENYEKITI wa Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt Mwinyihaji Makame Mwadini akieleza jambo mara baada ya kusomwa kwa maelezo mafupi juu ya uwekezaji wa maeneo huru ya vitega uchumi Micheweni.(PICHA NA ABDI ZULEIMAN, PEMBA)  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.