Habari za Punde

Wenye ulemavu kusaidiwa kupata mikopo

Na Takdir Ali na Amina Mkubwa.                                            
Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya maadili ya viongozi wakuu Serikali katka Baraza la Wawakilishi imesema itaendelea kuwatetea Watu wenye ulemavu ili waweze kupata mikopo ya kuendesha miradi ya kimaendeleo wanayoianzisha.
Akizungumza katika ziara ya kukagua vikundi vya Wajasiriamali kwa watu wenye ulewavu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Panya Ali Abdallah amesema watu wenye ulemavu wamekuwa wakianzisha miradi mingi ya kiuchumi lakini imekuwa haifikii malengo kutokana na ukosefu wa Wafadhili.
Amesema sababau kubwa inayopelekea miradi hiyo kutofikia malengo ni pamoja na ukosefu wa masoko ya uhakikika ya kuuza bidhaa wanazozizalisha na uhaba wa mitaji.
Aidha amewataka kubuni bidhaa kama vile mikoba yenye nembo ya Zanzibar ili waweze kuiuza kwa watalii na kujipatia kipato cha kujikimu katika maisha yao ya kila siku na kuepukana na hali tegemezi walionayo miongoni mwao.
Mh.Panya amewapongeza kwa juhudi wanazozichukuwa za kuanzisha miradi ya maendeleo na kuwataka wasivunjike moyo kutokana na matatizo yanayowakabili.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Watu Wenyeulemavu Abeidah abdallah amesema Watu hao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu hasa vijijini hivyo ni matumaini yao kuwa ujio wa kamati hayo utaweza kuwa chachu ya kutatua matatizo hayo yanayowakabili.
Amesema baada ya kuwaona wanakikundi hao wa Tumuamini Mungu Kivunge Wilaya ya kaskazini “A” wakipata usumbufu waliamua kukabidhi sh.laki 8 na ndio walipoamua kuanzisha ushirika huo unaojishughulisha na ufumaji wa mashuka,mazulia na usukaji wa makawa na mikoba.
Mapema wakitoa maelezo wanakikundi hao wamesema mtaji huo wa laki 8 ni mdogo na kuiomba kamati hiyo kuwasaidiwa angalau kiasi cha sh. milioni mbili zitakazoweza kuwasaidia kukuza mradi huo.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.