Habari za Punde

Mkenya Kipchoge aibuka kidedea London Marathon Avunja Rekodi ya Dunia

Rekodi mpya ya mbio za mwaka huu za Berlin Marathon, imechukuliwa na mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchoge, ambaye anakimbia mbio za masafa marefu kwa kasi zaidi duniani.
Bingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge mwenye umri wa miaka 33, ameweka muda mpya wa saa 2, dakika 6 na sekunde 39 na kuvunja rekodi ya mwenzake wa Kenya Dennis Kimetto aliyeweka rekodi mpya ya dunia ya saa 2, dakika 2 na sekunde 57 aliyokimbia mwaka wa 2014 katika mbio hizo za Berlin marathon.
Nyota huyo wa mbio ndefu amevunja rekodi ya mbio hizo kwa kutimka kilomita 42 kwa muda wa saa 2 dakika 1 na sekunde 40.
Hii ilikua ni mara ya tatu kwa Kipchoge kuibuka mshindi kwenye mbio hizo za Berlin marathon.
ipchoge amevunja rekodi ya Dunia kwa dakika 1 na sekunde 17, rekodi iliyoandikishwa na mkenya mwengine Dennis Kimetto, ya saa 2, dakika 2 na sekunde 57, mwaka 2014.
Nafasi ya pili na tatu ya mtokeo ya mbio hizo za Berlin Marathon, imenyakuliwa na wakenya pia.
Amos Kipruto aliibuka wa pili kwa saa 2, dakika 6 na sekunde 24.
Naye Wilson Kipsang akaibuka wa tatu kwa kutimka kwa saa mbili, dakika 6 na sekunde 48.
Ushindi wa mwaka huu wa mbio hizo upande wa wanawake, umenyakuliwa tena na mkenya Gladys Cherono.
Cherono alihifadhi ubingwa wake kwa muda mpya wa Berlin marathon wa saa 2, dakika 18 na sekunde 11.
Wakimbiaji wa Ethiopia Ruti Aga na Tirunesh Dibaba walimaliza wa pili na wa tatu katika mbio hizo za Berlin marathon.
Hivyo mashindano hayo ya marathon yaliyofanyika Berlin ,wakenya wamechukua nafasi tatu za mwanzo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.