Habari za Punde

Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar Waaza Leo Katika Majengo ya Baraza Chukwani Zanzibar.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza Chukwani Zanzibar leo. Wakati wa Mkutano wa  Kumi na Moja wa Baraza la Tisa  la Wawakilishi kwa kuwasilishwa Miswada Mitatu na Maswali na Majibu 154 kuulizwa na Wajumbe wa Baraza na Kujibiwa na Mawaziri wa Wizara husika wakati wa mkutano huo uloaza leo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Shamata Shaame Khamis akijibu Maswali yalioulizwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa Maswali na Majibu asubuhi katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja Baraza la Tisa la Wawakilioshi Zanzibar linalofanyika katika majengo ya Baraza Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Nadir Abdul-latif  Yussuf, akiuliza swli wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara husika katika Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar linalofanyika katika majengo ya baraza chukwani Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Mhe,Juma Makungu Juma akisisitiza jambo wakati akijibu maswali yalioulizwa na Wajumbe wa Baraza wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililoaza leo Zanzibar.
Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Idrisa Muslim Hija wakifuatilia michango ya Wajumbe wakati wa kuchangia Mswada wa Wazira ya Elimu baada ya kuwasilishwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, kwa Wajumbe leo katika Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.