Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Atoa Ahadi Kwa Timu za Mkoa wa Mjini Magharibi Zitakazofanya Vizuri Katika Tamasha la Kitaifa la Elimu Bila Malipo Zanzibar Kuwazawadia Kila Mchezaji Shilingi Laki Moja.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimkabidhi Kombe la Ubingwa la Michuano ya Tamashala la Elimu Bila Malipo Bingwa wa Mkoa wa Mjini Magharibi Kepteni wa Skuli ya Haile Sellasie Fauzi Abdallah, kwa kuibuka mshindu wa Fainali ya mchezo huo wa Basketi Ball baada ya kuifunga Timu ya Sekondari ya Nyuki kwa Vikapu 37 - 23. Mchezo uliofanyika Uwanja wa Maisara Zanzibar.

Wachezaji wa Timu ya Sekondari ya Haeli Sallesie wakivisha Medali zao za Ubingwa wa Basketi Ball Mkoa wa Mjini Magharibi Michuano ya Tamasha la Elimu Bila Malipo Zanzibar mchezo uliofanyika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Basket Ball kwa Wanawake Kepteni wa Skuli ya Sekondari ya Regeza Mwendo Calolira Timotho.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Basket Ball kwa Timu za Msingi Mkoa wa Mjini Magharibi Kenpeni wa Skuli ya Msingi ya Kijichi Innocent Epithasi Rajab. baada ya kuibuka Mabingwa wa Mchezo huo kwa Skuli za Msingi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.


Wachezaji wa Timu ya Skuli ya Sekondari ya Haeli wakishangilia wakati wakikabidhiwa Kombe lao la Ubingwa wa Mchezo wa Basket Ball kwa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.