Habari za Punde

NHIF Tanga Yapiga Kambi Wilayani Kilindi Kuhamasisha Mpango wa Toto Afya Kadi.

 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kuwaingiza watoto wao kwenye Mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kupaa huduma za matibabu wanapougua kwenye kijiji cha Gitu wilayani Kilindi mkoani Tanga
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu kwa muuza nguo kwenye soko la Gitu wilayani Kilindi mkoani Tanga juu ya umuhimu wa kuwaingiza watoto wao kwenye mpango wa Toto Afya kadi wakati wa uhamasishaji wa mpango huo
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga{NHIF) Ally Mwakababu akitoa elimu kwa wakazi wa Kijiji cha Gitu wilayani kilindi kuhusu umuhimu wa Toto Afya kadi kwa ajili ya watoto wao ili waweze kunufaika na matibabu wanapougua
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga{NHIF) Ally Mwakababu katikati akitoa elimu kwa wakazi wa Kijiji cha Gitu
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga{NHIF) Ally Mwakababu akitoa elimu juu ya umuhimu wa Mpango wa Toto Afya Kadi kwa mkazi wa Kijiji cha Gitu wilayani kilindi juu umuhimu wa watoto wao wakati wanapougua wakati wa uhamasishaji huo
 Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Macrina Clemens kushoto akihamasisha mpango wa Toto Afya Kadi kwa wananchi wa Kijiji cha Gitu
 Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Macrina Clemens akigawa vipeperusi kwa watoto vinavyoelezea mpango wa Toto Afya Kadi wakati wa uhamasishaji wa mpango huo
 MUUGUZI wa Afya akimpima mkazi wa Kijiji cha Gitu wilayani Kilindi
Mratibu wa NHIF wilaya ya Kilindi katika akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Gitu kushoto ni Mhasibu wa NHIF mkoani Tanga Hellena Manyanda
Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Macrina Clemens kulia akichukua maelezo ya mkazi wa Kijiji cha Gitu ambao walijitoikeza kwa ajili ya upimaji wakati wa uhamasishaji wa mpango wa Toto Afya Kadi wilayani Kilindi
 Mmmoja wa wahudumu wa Afya akimpima mmoja wa wakazi wa kijiji cha Gitu wilayani kKilindi
Sehemu ya wananchi wakisubiri huduma ya Upimaji wakati wa uhamasishaji wa Mpango wa Toto Afya Kadi katika Kijiji cha Gitu wilayani Kilindi Mkoani Tanga uliofanywa na NHIF mkoani Tanga.



Na.Mwandishi Wetu - Kilindi.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga(NHIF) umepiga kambi Kijiji cha Gitu wilayani Kilindi mkoani humo kuhamasisha umuhimu wa mpango wa Toto Afya kadi kwa wananchi ili kuwawezesha watoto wao kupata matibabu wanapougua.

Uhamasishaji huo ulifanywa na Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Ally Mwakababu akiwa ameambatana na watumishi wengine wa mfuko huo ambao walitembelea maeneo mbalimbali wilayani humo.

Akizungumza wakati akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wakiwemo watoto wao ambao utawasaidia kuweza kupata huduma za matibabu wakati wanapougua 

Meneja Mwakababu alisema suala hilo ni muhimu kwa watoto wao hususani wakati wa ukuaji wao kutokana na kukabiliwa na magonjwa mbalimbali hivyo mpango huo utawasaidia wazazi kuondokana na gharama za matibabu

“Kama unavyojua huu mpango wa Toto Afya Kadi ni mzuri na unampa uhakika mtoto wako kuweza kupata huduma za matibabu pindi wanapougua kwani sio nyakati zote wanaweza kumudu gharama za matibabu kutokana na kupanda kila wakati”Alisema.

Hata hivyo aliwataka pia wananchi wa Kijiji hicho kuona namna bora ya kujiunga kwenye mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapokumbana na magonjwa mbalimbali.


Uhamasishaji huo unafanyika umefanywa na mfuko huo kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ili kuwawezesha wananchi kuchangamkia fursa hiyo wa kujiunga na mpango wa Bima ya Afya wao na Watoto wao

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.