Habari za Punde

Timu ya Mlandege Yatinga Robo Fainali Michuano ya Ujamaa Sports Club Baada ya Kuifunga Timu ya Muembeladu Kwa Mabao 2-1 Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Ikiungana na Timu ya Taifa ya Jangombe, Malindi na Timu ya Rastazoni Katika Mchezo wa Robo Faina Kesho.

Wapenzi wa Timu ya Mlandege wakifuatilia mchezo wa Timu yao  ya Michuano ya Kombe la Ujamaa Sports Club dhidi ya Timu ya Muembeladu Sports Club uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Mlandege imeshiba bao 2-1.

Timu ya Mlandege imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya mchezo wa Robo Fainali kuungana na Timu za Taifa ya Jangombe. Malindi na Timu ya Rastazoni michezo hiyo kufanyika kesho katika Uwanja wa Amaan saa 10.00 jioni kwa mchezo wa kwanza utakaozikutanisha Timu za Malindi na Mlandege.

Mchezo huo wa Robo Fainali ya Michuano ya Ujamaa Cup utakuwa na upinzani mkali kutokana kwa Timu hizo zote mbili zimepanda Daraja la Kwanza Taifa kwa msimu huu wa 2018/2019, na utaleta upinzani kutokana na upinzania wao katika daraja waliotoka.
Robo Fainali ya Pili itafanyika keshokutwa kwa mchezo wa Taifa ya Jangombe na Rastazoni saa 10-00 jioni katika uwanja huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.