Habari za Punde

Usafiri wa Pikipiki Maarufu Kwa Jina la Bodaboda Visiwani Zanzibar Mkombozi wa Wananchi Kurahisisha Safari Zao.

Vijana waendesha pikipiki maarufu kwa jina la Daladala wakiwa katika kituo cha gari za abiria kikwajuni wakisubiri wateja wao ili kutowa huduma hiyo, kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika eneo hilo.  

Wananchi takribani alilimia 85 kisiwani Zanzibar hutumia usafiri wa Pikipiki maarifu kwa jina la Bodaboda hutowa huduma hiyo kwa wananchi katika safari za hapa na pale kutoka na urahisi wake wa bei huchajia kutokana na umbali wa safari yako.

Vijana wengi kisiwani Zanzibar wamejiajiri kupitia kazi hiyo ya kusafirika Wananchi kwa kutumia pikipiki katika maeneo ya vituo vya daladala hukaa na kusubiri abiria wao ili kutowa huduma hiyo, kwa bei ya maelewano kwa usafiri wa mjini kuazia katika kituo cha daladala michezani na kikwajuni kuelekea mji mkongwe hadi bandari huchukua kuazia shilingi 2000/ na 2500.

Usafiri kwa sasa umekuwa mkubwa hadi katika vituo cha gari za abiria mashamba nako hukaa katika vituo hivyo kutowa huduma hiyo kwa wananchi wanaofika na kuwafikisha katika makaazi yao umbali na kituo cha daladala.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.