Habari za Punde

Viongozi wa Vyama Vya Michezo Zanzibar Wapaigwa Msasa na TOC.


Viongozi wa Vyama vya Michezo Visiwani Zanzibar wametakiwa kuimarisha michezo yao kwa kuisambaza kwenye Wilaya zote za Unguja na Pemba ili Wananchi wapate fursa ya ajira.
Akifunga mafunzo ya Viongozi wa Michezo huko Rahaleo katika ukumbi wa Sanaa, Mkurugenzi wa Michezo na Utamaduni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amaali Zanzibar Hassan Tawakal Hairallah amesema Mafunzo vyama vya michezo wanajukumu kubwa la kuleta maendeleo ya Michezo hivyo wanapaswa kufanya jitihada za kuisambaza Zanzibar nzima kwa kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo kutoka Kamati ya Olympik Tanzania (TOC)  Suleiman Mahmoud Jabir amesema ataendelea kutoa ushirikiano wake kwa kutoa mafunzo mbali mbali huku akiwataka viongozi hao kuyafanyia kazi mafunzo hayo na kujipanga upya ili kuleta maendeleo ya michezo zanzibar.

Nao washiriki wa Mafunzo hayo ya wamesema wataenda kuyafanyia kazi na kufata taratibu zote za uongozi ili kuepusha migogoro mbali mbali inayojitokeza katika Vyama vyao.

Mafunzo hayo ni ya wiki moja ambayo yametolewa na Kamati ya Olmpik Tanzania (T.O.C) yakijumuisha jumla ya viongozi 27 kutoka vyama sita tofauti vya michezo vikiwemo chama cha Mpira wa Pete, Kikapu, Meza, Riadha, mpira wa mikono na mpira wa ukuta.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.