Habari za Punde

Wazazi na Walezi Watakiwa Kutowa Ushirikiano na Serikali Katika Vitendo Vya Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akifungua Mkutano wa Wazi wa Kutowa Maoni Wananchi kuhusiana na Kupokea Maoni ya Wananchi Dhidi ya Mapambano ya Ukatili na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar ulioandaliwa na Zizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar, uliofanyika katika viwanja vya Watoto Kariakoo Zanzibar kushoto Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Mhe. Shadya Mohammed na kulia Mshauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Masuala ya Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar

Na.Khadija Khamis –Maelezo 16/9/2018.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Mhe, Riziki  Pembe Juma aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano na Serikali kuhakikisha vitendo vya uzalilishaji vinaondoka nchini .
Hayo alisema leo huko katika kiwanja cha kufurahishia watoto kariakoo wakati wa mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya wananchi dhidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wanawake na watoto ulioandaliwa na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto..
Alisema serikali imetunga sheria kwa wale wote wanaofanya vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto lakini kila siku vitendo vinaendelea hivyo iko haja ya mashirikiano ya pamoja kati ya walezi wazazi na serikali ili kuvidhibiti vitendo hivyo .
Aidha alisema tupange mikakati madhubuti kwa pamoja jinsi ya kuondoa wimbi sugu la udhalilishaji wanawake na watoto na hata watu wazima na kuhakikisha kila mmoja anahusika katika mapambano ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia ..
Nae mshiriki wa mdahalo huu Shadida Machano alisema wazazi wawe karibu na watoto wao na kuwalea malezi ya kirafiki ambayo yanazingatia maadili ili kumjengea mtoto uwezo wa kusema kwa kila ambalo linamtokezea .
Alisema skuli ziandaliwe masomo maalumu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari ili kuweza kujielewa na kujihami.
Hata hivyo alisema ingawa jamii imeharibika kwa kiasi kikubwa kutokana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hivyo iko haja walimu wa skuli pamoja na  madrasa kupewa mafunzo maalumu.
Nae mshiriki wa mdahalo huo kheir Miraji othmani wa Chukwani alitoa rai ya nini kifanyike ili kudhibiti vitendo hivi alisema itolewe adhabu ya mara moja  uliyo madhubuti kwa haraka .
“Amekutwa pale pale avuliwe nguo apigwe mikwaju katikati ya umati wa watu, kwani yeye si  kadhalilisha basi adhalilishe,afungwe kifungo ch maisha. “ alisema kheir Miraji mmoja wa wazazi.
Bi Raya Mohamed Sleiman wa Mchangani alieleza hali halisi  ya kukosa mashirikiano kwa polisi na mahakama jambo ambalo linavunja moyo na kurejesha nyuma juhudi za kupiga vita vitendo hivyo.
  “Tatizo hatuna nia ya dhati kuliondoa hili jambo kwa sababu kwa nini tunalindana? udhalilishaji imekuwa kama biashara ya kujiingizi fedha kwa njia ya ruchwa hivi kweli muhalifu anatoroka kituoni “alisema bi Raya.
Alisema sheria zinaachwa katika makaratasi hazitekelezwa hii inaonyesha wazi huu ni mtandao maalum ambao kama serikali ipo tayari kuuvunja unaweza kwani ushahidi umeonyesha imepiga vita mifuko ya plastic imeweza helment imeweza na hili haishindwi .
Nae Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Mhe,Maudline Castico alitoa wito kwa wazazi na walezi kuvuata maadili katika malezi na makuzi ya watoto ili kujenga maandalizi mema kwa ajili ya taifa la kesho.
Nae Jaji Mshebe Ali Bakari alieleza suala la kuporomoka  kwa maadili kwa vijana na watoto kunachangia kuimarisha vitendo vya udhalilishaji hivyo iko haja ya wazazi na walezi kurekebisha maadili ilI kuzuia udhalilishaji kwa pamoja Baina ya wazazi na serikali .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.