Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Afungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Alat Jijini Dodoma leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete kufungua Mkutano wa 34, wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa, Septemba 27, 2018.  Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa. Watatu kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege na watatu kulia ni Meya wa jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu mitambo ya umeme kutoka kwa Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa Tekinolojia na Masoko wa REA, Elineema Mkumbo (wapili kushoto) wakati alipotembelea banda la maonyesho la REA kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Kwenye ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma 
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akifungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT)  kwenye ukumbi wa Jakaya  Mrisho Kikwete jijini Dodoma 
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye  ukumbi  wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma, 
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Jumuiya ya Tawala za Mitaa Alat baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo wa 34 uliofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) Kwenye ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma Septemba 27, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa ALAT, Gulaam Hafeez 'Mukadam',   wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na wanne kulia  ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.