Habari za Punde

Waziri Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Azungumza na Kamishna wa Taasisi ya Takukuru

Na. Raya Hamad OR KSUUUB
Imeelezwa kuwa lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar  litatimia iwapo mashirikiano na maelewano yaliyopo yataendelezwa  ili kuleta ufanisi na tija kwa Muungano wetu 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe Haroun Ali Suleiman alipokutana na Mkurugenzi  wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Tanzania Bara Kamishna Diwani Athumani Ofisini  akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar ZAECA  “ziara Mussa Haji ALI kwake  Mazizini   

Waziri Haroun amesisitiza kuwepo kwa  mashirikiano baina ya  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar ZAECA  “ziara za kutembeleana na kubadilishana mawazo na uzoefu zinaleta  umoja  na tija kwa Taifa kulingana na majukumu ya taasisi hizi ni mazito  lakini isiwe sababu ya kuwa ni kikwazo cha kutimiza wajibu wenu na ndio maana mkaaminiwa na viongozi wanchi “alisisitiza 

Vita ya kupambana na  kuzuwia rushwa na uhujumu uchumi  ni kubwa iliyoota mizizi  hivyo taasisi zote mbili zinawajibu wa kutoa taaluma kwa taasisi za umma na  jamii ili kwenda sambamba na kasi ya uwajibikaji hasa kwa ulimwengu huu wa sayansi na teknologia .

Mhe Haroun amewasisitiza viongozi wote wawili wa ZAECA na TAKUKURU  kuendeleza utamaduni wa kubadilishana uzowefu wa kiutendaji na kutumia mbinu za kisasa za kupambana na rushwa kwa kuwashirikisha wafanyakazi wao na kuwapa mafunzo ya ndani na nje , kukuza uhusiano na kushiriki  makongamano mbali mbali yanayoandaliwa kitaifa na kimataifa  .

Akitoa shukurani zake Mkurugenzi TAKUKURU Kamishna Diwani Athumani  ameahidi kuendeleza uhusiano uliopo na kuendeleza mapambano dhidi ya Rushwa kwa mashirikiano ya  pande  zote mbili kwa vile Taasisi hizo zina jukumu moja la kudhibiti vitendo vya rushwa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.