Habari za Punde

Zoezi la Uokaji Likiendele Katika Ziwa Victoria Mwanza.

Waokoaji wakiwa katika zoezi hilo pembezoni mwa kivuko hicho cha Mv Nyerere kilichopinduka na kupelekea maafa ya Wananchi waliokuwemo katika kivuko hicho kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa ,katika eneo la ukara ,kisiwa cha Ukerewe jijini Mwanza, wakiendelea na zoezi hilo kutafuta miili ya abiri wa kivuko hicho.

Mv Nyerere hufanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika Wilaya ya Ukerewe mkoani mwanza, kilipata ajali alhamishi ya wiki hii septemba 20/9/2018 kikikadiriwa kubeba abiria idadi kubwa kuzidi uwezo wake.

Kwa Mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, mpaka wakati huu tayari miili ilioopelewa majini imefikia 209, kati yao miili 172 imetambuliwa na ndugu zao na 112 ikiwa tayari imeshachukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya maandalizi ya maziko (Picha zote na Steve Magombe AKA Kasampaida) 
Vivuko vya Mv Clarias na Mv Nyehungue vikishiriki katika zoezi hilo kwa kutowa msaada wakati wa uokozi huo.
Vijana wa Red Cross wakishiriki katika zoezi hilo la Uokozi. 
Vijana wa Red Cross wakishiriki katika zoezi hilo la Uokozi.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama na Wananchi wakiendelea na zoazi hilo la kuokoa miili ya marehemu waliopata ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere katika ziwa victoria Mwanza likiendelea.  
Zoezi likiendelea katika Ziwa Victoria kuopowa miili ya marehemu waliopata ajali hiyo ya Kivuko cha Mv Nyerere Mwanza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.